News
Loading...

Uzinduzi wa kampeni jana UKAWA Sumaye aijibu CCM!



Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani mapema leo.Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.


Aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya pili Mh Fredrick Sumaye jana alipangua shutuma za CCM dhidi ya mgombea u rais wa UKAWA Mh Edward Ngoyai Lowassa. Akihutubia maelfu ya watu waliojitokeza katka viwanja vya jangwani jana Mh Sumaye alisema "Wanamtuhumu Lowassa kuwa ni fisadi mkubwa, lakini mmi nahoji angekuwa fisadi si wangeshamweka mahali? Na tangu atoke madarakani ni miaka nane sasa mbona hajakimbia nchini? Akaongeza "Wakati ufisadi wa EPA unatokea Lowassa alikuwepo?
wakati twiga wanapandishwa ndege Lowassa alikuwepo? Na ufisadi wa ESCROW unatokea Lowassa alikuwepo? Mbona hayo hawayasemi? Alisema huku akishangiliwa mno na umati huo uliofurika katika viwanja vya jangwani jijini Dar.

Tuhuma nyingine aliyoipangua Sumaye ni kuwa Lowassa ni mgonjwa, alisema "Mbona Mh Mkapa alifanyiwa oparesheni kubwa tu wakati wa utawala wake? Na mbona Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume? akaongeza kazi ya rais sio kubeba zege Ikulu bali anatakiwa awe na timu nzuri ya kumfanyia kazi na si zaidi.

Akihutubia umati huo mgombea u rais wa UKAWA Mh Lowassa alisema kipaumbele katika ilani ya UKAWA ni elimu elimu na elimu kwa kuwa nchi yetu bado ipo nyumba katika nyanja hiyo.
Vile aliahidi iwapo ataingi Ikulu baada ya uchaguzi atawatoa kifungoni masheikh waliofungwa huko Zanzibar.

Hata hivyo Mgombea huyo wa urais kupitia UKAWA aliongea kwa dakika 12 tu kutokana na ufinyu wa muda ambapo baadae aliisoma hotuba yake katika kipindi maalum kupitia kituo cha runonga cha ITV cha jijini Dar es Salaam.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani leo.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzimduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani leo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea urais kwa Upande wa Zanzibar na Upande Wa Bara na mgombea mwenza bara wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za ukawa uliofanyika katika viwanja vya jangwani.
Halima Mdee akihutubia
 
 Wagombea Ubunge katika majimbo ya Dar Es Salaam wakitambulishwa mbele ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo zilizofanyika katika Uwanja wa Jangwani.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya CUF Kingwendu akisikiliza hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Mwamvuli ya Ukawa
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza leo katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jangwani jijini Dar
 Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Fredrick Sumaye akihutubia wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa
 Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya jangwani leo
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema na Mgombea Mwenza wakiwaaga watanzania waliojitokeza katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa
Moja ya kifaa cha Kisasa kabisa aina ya Drone ambacho kilikua kikitumika kupiga picha kutoka angani ambacho kimekuwa kivutio kikubwa kabisa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo katika viwanja vya jangwani . 

Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :