News
Loading...

Wazee wa baraza na usalama wao


ITAWEZEKANAJE? Hivyo ndivyo inaelekea
ndugu hawa wa marehemu wanajiuliza kivipi wazee wa
baraza wakawakosa na hatia watuhumiwa wa mauaji ya
 Swetu Fundikira?
Tangu wiki iliyopita tarehe 4/June nimekuwa nikihudhuria mahakamani katika kesi ya mauaji ya Swetu Ramadhani Fundikira mpaka jana tarehe 12/06 ilipofikia ukomo kwa siku ya hukumu kutajwa kuwa ni 30/10/2012, sio siri nimefumbuka mno na weledi unaotumika humo katika kuendesha kesi hasa ya mauaji. Lakini kuna suala moja linanitatiza nalo ni usalama wa wazee wa baraza, wamekuwa wakifika pale mahakamani kwa dala dala na wamekuwa wakiondoka hapo kwa daladala. Tujiulize watu wanaopewa jukumu kubwa la kutoa maoni yao katika kesi ya mauaji kupatikana kirahisi namna hiyo ni sawa? Nasikia wanalipwa sh 10,000/= kila siku watakayohudhuria mahakamani. Je ni sawa kuweka maisha ya mtu hatarini kwa kumlipa sh 10,000/= tu? Je tunawezaje kusema kuwa ndugu wa washtakiwa hawawezi kujaribu kuwarubuni wazee hawa? Nchi zilizopiga hatua wazee hao huwekwa kambini kwa kipindi chote cha kesi itakapokuwa ikiendelea, hivyo basi huwa salama na watatarajiwa watoe maamuzi yenye kuzingatia haki.
Kwa mtazamo na mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo;

1.Ipo haja wazee hawa wafanyiwe mchujo ikiwezekana na wajaribiwe ili kujua uwezo wao wa uelewa na busara, kwani si kila Mzee ana busara.
2.Wawekwe kambini kwa siku zote watakazokuwa wakisikliza kesi kabla ya kutoa maoni.
3.Wafikishwe mahakamani kwa usafiri maalumu na warudishwe kambini na usafiri huo.
4. Waongezwe posho hata ifikie 50,000/= kwa siku.
Yangu ni hayo tu kwa sasa

Ndugu wa marehemu Swetu Fundikira wakiwa nje ya mahakama jana


Ndugu wa marehemu mahakani

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :