News
Loading...

Enough is enough! Ni wakati muafaka kambi za jeshi zihame mjini!


HUU NI MOJA WA MILIPUKO YA JANA HUKO UKONGA

Ikiwa ni takriban miaka mitatu tangu kambi nyingine ya jeshi ilipuke huko Mbagala na kusababisha maafa makubwa ikiwa na pamoja na vifo kwa wakazi wanaoishi maeno yanayoizunguka kambi hiyo ya JWTZ, na jana usiku yamejirudia yale yale mabomu yamelipuka katika moja maghala ya JWTZ na yamesababisha maafa makubwa pamoja na vifo vya watu wasiopungua kumi na saba hivi kwa mujibu wa runinga la TBC1. Sasa mimi nafikiri wakati umefika sasa hawa mabwana wafunge virago vyao wahamie maporini ili kuepusha maafa mengine yasije yakajitokeza katika kambi nyingine kama Lugalo, Mbweni na zingine nyingi zilizo maeneo ambayo raia wanaishi. Najua wao wakiambiwa kuhama husema kuwa kuwa hawawezi kutokana na vitu vilivyomo katika kambi hizo kamwe hawawezi kuviacha nyuma au havihamishiki. Lakini wanapaswa wajue milipuko kutokea na kuathiri na maisha ya raia na mali zao ni jambo la hatari kuendelea kuruhusiwa litokee huku kukiwa na uwezekano wa kuhamisha makambi hayo ya wababe hawa ambao huamini wapo juu ya sheria kote barani Afrika ni jambo la aibu kubwa kwa serikali na wizara ya ulinzi. Ni juu ya serikali sasa kuwashaiti mabwana hawa wahame.
picha kwa hisani ya michuzi junior.blogspot.com

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :