|
Tunguri juu ya tunguri |
Msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flava Hamisi Mbizo aka H-Mbizo hatimaye leo hii jumamosi ameanza kuchukua picha za video ya wimbo wake mpya Mvute mvute, Hmbizo ambaye amewahi kutamba na nyimbo kama Mchumba na Kunguru
alipotea katika anga la muziki huo wa Flava za Bongo ameibuka upya na
wimbo huo Mvute mvute ambao anamzungumzia msichana anayempenda lakini
kila akimtokea mrembo huyo amekuwa akimpiga na chini kiasi kwamba
akaamua amuendee kwa mganga wa kienyeji ili amtie ujinga aweze
kumkubali yeye. Katika video hiyo amemshirikisha pia mkali wa vichekesho
Bambo ambaye ndiye anacheza kama mkware anayeamua kumroga binti wa watu
Samia baada ya kumkataa Pia sehemu ya mganga inachezwa na msanii wa
maigizo kwa jina Ndemele, yeye huyu ni msanii anayeigiza kama mganga wa
kienyeji hivyo basi ili kujenga uhalisia ana kila kitu ambacho mganga wa
kweli wa kienyeji huwa anvyo navyo ni kuanzia noti zamani mpaka tunguri
za aina mbali mbali. Jionee mwenyewe pichani. HMbizo alipoulizwa anafanya video na kampuni gani bado hakuwa tayari kuitaja ila alisema nawaomba mvute subira baada ya siku tano hivi tutajua nani atakuwa ndiye liyeifanya video hii ya Mvut mvute.
|
Hiki ndicho kilinge cha bwana Ndemele. |
|
Hii ni shilingi ishirini nyekundu na yenye picha rais mstaafu |
|
|
Shilingi mia moja ya noti nyekundu. |
|
Hii ni sh ilingi ishirini ya miaka ya mwanzoni ya uhuru. |
|
Hawa na Samia. |
|
Hawa, Bambo na Samia baada ya kumaliza shooting. |
|
Kutoka kushoto ni Hawa, Bambo, Samia na HMbizo. |
|
Samia, ndiye mrembo anayemdatisha Bambo. |
FACEBOOK COMMENT
Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
.
0 comments :
Post a Comment