News
Loading...

Mlipuko wa mkubwa wazua kizaa zaa Kinondoni Morocco!


Hii ndiyo Transforma iliyolipuka.

Leo hii majira ya saa tano asubuhi maeneo ya Kinondoni Morocco palitokea patashika ambapo kwa muda wa kama dakika moja tu watu walikmbia huku na kule baada ya kusikika mlipuko mkubwa mithili ya yale mabomu yaliyolipuka juzi katika kambi ya JWTZ huko Gongo la Mboto na kupelekea wakazi wa maeneo hayo na yale ya jirani kuyakimbia makazi yao kwa muda wa saa 24. Mlipuko huu wa leo ulikuwa ni wa Transforma ya Tanesco iliyopo jirani na Makao makuu ya Airtel Kinondoni Morocco, eneo ilipo nguzo hiyo iliyolipuka ni maarufu kwa wachuuzi wa viatu na nguo mtumba,vocha na vinwyaji baridi nk. Baada ya mlio huo wachuuzi hao walikimbia umbali mfupi tu kabla ya kubaini mlipuko huo ulikuwa wa transforma ndipo wakageuza na kurejea katika vibanda vyao. Baadae ilithibitika kuwa mlipuko huo huo ulipelekea katikizo la umeme maeneo ya Kinondoni Bwawani na maeneo mengine ambapo hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida katikizo hilo halikudumu kwa muda mrefu sana  kwani baada ya kama masaa mawili hivi huduma hiyo adimu kwa wa Tanzania ilirejea, angalau kwa wakati huu. Ama kweli ukiumwa na nyoka!
Makao makuu ya Airtel Kinondoni.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :