Wapendwa wadau kama isomekavyo hapo juu, katika makala fulani hapo nyuma niliwaulizeni juu ya kubadili jina la blog hii kutoka keronyingi.blogspot.com kwenda mkalafundikira.blogspot.com na sababu nilizieleza. Kimsingi mimi sina tatizo na jina alimradi ninyi wadau mnaridhika, tangu jana nimepokea maoni kadhaa juu ya suala hili na wengi wenu mnapendekeza jina libaki hili hili la keronyingi.blogspot.com. Lakini pana mmoja wenu ametoa maoni yake na kuuliza nini mantiki ya mimi kutumia jina keronyingi ilihali zinaingia habari hata zisizo na kero? Huyu mdau alitoa maoni hayo ana point, labda tu nikiri kuwa nilipoanzisha blog hii nilisukumwa na kero kadha wa kadha nizionazo mitaani,serikalini na kwingineko kwingi. Lakini pia napitia blogu za watu wengine na naona kuwa wengi hawa post vitu viendanavyo na majina ya blogu husika. Kwa kusema hivi si kwamba natafuta njia ya mkato kuondokana na mjadala huu, la hasha, bado napokea maoni na tutaendelea kuyajadili humu. Lakini pia napenda kuwahakikishieni kuwa msimamo mkuu wa blogu hili ni kukemea kero zozote zitokeazo hilo halitobadilika kamwe.
Keronyingi au Mkalafundikira.blogspot.com?

0 comments :
Post a Comment