News
Loading...

Madereva wa Tanzania walivyokosa uelewa!


Hapa ni maunganiko ya mitaa ya Livingstone na Uhuru jioni hii.



Wengi wa madereva wa Tanzania inaelekea wanaendesha magari bila ya kujua sheria za usalama barabarani ama hata kuwa na uelewa wa kawaida tu (common sense)kwa mfano hiyo picha kushoto inaonesha daladala likiwa limesimama katika foleni kwenye barabara ya Uhuru na kuziba kabisa njia kwa magari yenye kuelekea upande mwingine wa barabara huku dereva wa corona nyeupe akisubiri msamaria mwema ampishe aingie katika barabara hiyo au akatize kuelekea upande mwingine wa Mtaa wa Livingstone. Nimesema msamaria mwema ampishe kwa kuwa hapa Dar ukiwa kwenye situation kama hiyo ujue umekwisha, yaani madereva wanaokatiza hapo huwa kama umegombana nao ilhali hata hamjuani, wengine huongeza mwendo ili akuwahi wewe usipite. Wengine pamoja na kuwa barabara aliyopo yeye ina foleni , lakini yu radhi akifika katika junction azuie magari mengine yasipite mpaka foleni yake yeye itakapoanza kusogea. Sasa hili halifundishwi shule wala unapoanza kufundishwa kuendesha gari bali ni common sense na ustaarabu wa dereva husika ambao Kwa Dar labda ni asilimia tano ya madereva wote. Katika hali ya kawaida ukiikuta foleni imekaribia katika junction unaacha uwazi ili magari mengine yaendelee kupita na si kuzuia pale ili mkose wote. Kingine ni honi, yaani madereva hapa jijini wanapiga honi kana kwamba kila akipiga anapata robo lita ya petroli. Katika mataa ya barabarani ukiwa mbele na taa zikabadilika ghafla toka nyekundu kuwa kijani utapigiwa honi wewe utafikiri umechelewa kuondoa gari yako kwa sekunde kumi kumbe la! Nchi zilizoendelea hasa ulaya kama UK kwa mfano unaweza ukakaa hata miaka 2 usisikie mlio wa honi, wenzetu hawapigi honi kabisa, labda uwe taxi driver ndipo utapiga honi mara moja ukienda mchukua abiria wako kumfahamisha kuwa umefika. Au Pengine pawe na demonstaration na madereva waandaaji huwaambia madereva ifikapo saa flani tutapiga honi kwa sekunde kumi mfululizo, na watafanya hivyo tu si zaidi.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

hiyo kalii sana.

Anonymous said...

Always common sense haziko common