News
Loading...

Bongo flava Fc 2- 0 Bongo movie!


Kandanda inaendelea.
Leo hii katika uwanja wa taifa jijini Dar palikua na mpambano mkali baina ya timu za Bongo flava Fc na Bongo muvi Fc. Mpambano huo ulioandaliwa na Clouds tv na redio kwa dhumuni la kuchangia wahanga wa mabomu huko Gongo la Mboto. Timu ya Bongo Flava Fc ambayo iliundwa na wasanii wa muziki wa Bongo Flava ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa sufuri yaliyowekwa kimiani na Hamis Baba aka HBaba katika kipindi cha kwanza, HBaba pamoja na kufunga magoli hayo mawili hakuweza kumfunika Ally Kiba ambaya alicheza kama playmaker ndiye aliyempa pasi Hbaba kufunga bao la pili na hasa ndiye alikuwa nyota wa mchezo. Ally Kiba alionesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutoa pasi za uhakika. Kiasi kwamba nilifikiri akipenda anaweza kucheza mpira katika timu yeyote katika premier league na hii si blah blah huy kijana anaweza kucheza mpira. Kwa kweli kiwanjani hapo palikuwa na burudani ya aina yake pale Masanja mkandamizaji alipoingia uwanjani huku akionekana wazi hana lolote alijualo kuhusu mchezo huo wenye washabiki wengi zaidi duniani lakini alikonga nyoyo za mashabiki wapatao elfu 35 hivi waliofurika uwanjani humo kila alipobahatika kugusa mpira watu waliangua vicheko. Kuna wakati alijiandaa kupiga kichwa lakini akaukosa mpira akaamua kuunawa ndipo Mwamuzi Othman Kazi alipomfuata kumuonya Massanja akalala chini kisha akaanza kupiga puh ups na kupelekea Othman Kzi kuangua kicheko kwa muda. Timu ya Bongo muvi itabidi ijilamu baada ya kupoteza nafasi mbili za penati kwa kupiga nje mipira hiyo ya adhabu iliyopatika katika vipindi viwili vya mchezo huo. Walizawadiwa paenati hizo baada ya walinzi wa Bongo Flava kunawa mpira katika eneo la hatari hivyo Mwamuzi Othman Kazi kuamuru zipigwe penati ambapo Benny Kinyaia alikosa penelti ya kwanza katika kipindi cha kwanza. Pamoja na kufungwa magoli hayo mawili kipa wa Bongo Muvi ndiye alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ambapo alijizolea sh laki moja toka kwa mdhamini Othman Tippo aka zizou fashion. Pia timu ya Bongo Flava ilijipatia kombe na jezi seti moja to zizou fashion.
Huu ni umati uliofurika kushuhudia mchezo huo wa kirafiki.

Nyomi


Producer Lamar na Msanii Jaf-rhymes Jafari Mshamu.


Wasanii Amin kushoto na Mwasiti wa pili kulia waakifuatilia mchezo
Bongo Flava FC

Bongo movie FC


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :