News
Loading...

Uwanja wetu bora lakini si bora kivile!


Kwanza nitangulize shukurani kwa wale wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine mpaka hii leo tuna uwanja mzuri wa kuvutia na wa kujivunia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati. Lakini mara zote ninapoenda uwanja wa Taifa kutazama mechi mbali mbali hujiuliza "Hawa wahandisi walio uchora ule uwanja walifikiria nini hasa kwa 
1. Kutotenganisha milango ambapo wa VIP aliyelipa laki moja ghafla hujikuta kakaa na rafiki yake aliyelipa sh elfu tano. 
2.Kutoweka VIP ya viongozi wa nchi ambapo hata Mh Rais akizuka kuja kuona mechi  huwekewa office chairs yeye na msafara wake.
3. Kutoweka sehemu maalum za kuuzia vinywaji laini na vile vigumu nje ya sehemu za kukalia.
4. Kero hizi mbili zifuatazo haziwahusu wachoraji wa uwanja huu, (a)Upatikana wa taabu wa tiketi (b) uchache wa mageti yanayofunguliwa mara mechi inapomalizika. Sasa uwanja kama huu wenye mapungufu kama hayo unakuwaje bora? Ni jambo la kutia aibu kuona eti umefuatana na rafiki yako toka nyumbani yeye anakata tiketi ya sh 5000 na wewe sh laki moja na anakutambia hapo hapo kuwa utakuta naye VIP, na baada ya nusu saa kweli unashtukia unaguswa bega na ukigeuka unakuta ni yeye. Jingine ni lile la kutokuwa na VIP yenye hadhi hasa ya kuitwa VIP, wageni wa heshima wanawekewa office chairs halafu utasikia eti kuna mtu alifanya kazi bega kwa bega na hao wahandisi na akaridhika tu uwanja kuwa hauna vip seating area za viongozi huu ni upuuzi mtupu. Lingine ni kutokuwa na sehemu ambazo washabiki watajipatia japo bia mbili tatu kabla ya game na wakati wa mapumziko halikadhalika, viwanja bora vina hizo sehemu kwa mfano Old Trafford na vyote vingine nchini England. Salamu kwa wahusika
Tafadhalini mageti yafunguliwe mengi ya kutosha wakati mchezo unapomalizika, vinginevyo hiyo ni kuwatengenezea vibaka mazingira ya kuibia watu vijisenti vyao. Ukiufananisha na shamba la bibi na viwanja vingine Afrika Mshariki uwanja wetu ni bora pande hizi lakini si kiviile, umeona eeh?
Uwanja wa Taifa
Shamba la bibi.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :