News
Loading...

Chuki ya binadamu dhidi ya kunguru!Huyu ni kinda wa kunguru akionekana kuomba
 msaada,kwa aidha mama yake au tu kwa jamii
 ya kunguru waliopokaribu nahapo juu ya nyaya
 zaumeme kama waonekanavyo hapo chini.
Kwa bahati mbaya Kunguru si ndege mwenye marafiki wengi katika jamii ya wanadamu kwani kwa njia moja ama nyingine ameshawaudhi wengi kwa kifupi hapendwi hata kidogo. Pichani anaonekana kinda wa kunguru akiwa ardhini ambako haikufahamika mara moja alifikaje, nafikiri alikuwa katika mazoezi ya kupaa kama wengine na kwa bahati mbaya akaanguka.
Nilishuhudia mtu mzima ya mwenye umri juu ya miaka 18 akimpiga mateke kinda huyo, sikushangaa sana kwani ni wiki tu ilikuwa imepita tangu nishuhudie mtu mzima mwingine akiwasaidia watoto kumuangusha kinda wa kunguru toka mtini na alipofanikiwa watoto hao walimgeuza kunguru huyo mpira walimtesa mpaka akafa. Na wiki kadhaa zilizopita nilifika katika bar moja maeneo ya Kurasini nikakuta kunguru kaning'inizwa mtini kichwa chini miguu juu. Yote haya ni uthibitisho kuwa Kunguru hapendwi na hatakiwi na jamii ya wanadamu kutokana na matendo yake maovu, nayo ni pamoja na kunyea wenye nguo nyeupe,kunyakua vifaranga vya kuku na hata kupora nyama toka mikononi mwa binadamu na mengine mengi ambayo yamemfanya kuwa adui nambari moja wa binadamu. Pole kunguru,kazi unayo!


Kunguru hawa waliishia kupiga kelele
bila kutoa msaada wowote kwa kinda huyo. FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :