News
Loading...

Hali hii itaendelea mpaka lini?


Hapa ni Mwananyamala soko la Mapinduzi,
Hapa pamekuwa na kero iliyopitiliza, yaani ma daladala hapa husimama barabarani yanaposhusha ama kupakia abiria, hali hiyo huleta bugudha na kero za kupindukia kwa watumiaji wengine wa barabara hiyo. Na haielekei kama wahusika wameona kero mbayo hutokea mara konda fulani anapoamua kuwa anataka kubeba abiria wote waliopo kituoni hapo, na hivyo kusimama barabarani bila kujali anatengeneza foleni ya ukumwa gani. Msururu hujiunda kwa ghafla na katika kipindi cha dakika 2 au tatu tu huwa hapatamaniki. Msururu hufika hadi katika kona ya kuelekea Mwananyamala Hospital au kwa Kopa kwa kuelekea upande mwingine. Ninachopendekeza mimi, pahala hapa pajengwe maegesho ya vituo ambayo yatasaidia kupunguza kero katika eneo hili la jiji chafu yaani Dar es Salaam au kama hilo haliwezekani, basi pawekwe askari wa usalama barabarani ili atishe wavunja sheria mahali hapo waache kuunda misururu pasipo sababu. 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :