News
Loading...

Mzee Yusuf kurejea jukwaani!


Mzee Yussuf aka king of Taarab.
NI rasmi sasa kuwa Mfalme wa taarab nchini Mzee Yussuf anarudi jukwaani na onyesho lake la kwanza kabisa ni katika mkesha wa Valentine Day, Jumapili 13/2/2011ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel Mzee Yussuf aliyekuwa nje ya jukwaa kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia operesheni ya goti aliyofanyiwa katika hospitali ya Dk Baki huko Kibaha, atafanya makamuzi hayo na kundi lake la Jahazi Modern Taarab ambapo atatumia fursa hiyo kutambulisha vionjo vyake vipya.Mkurugenzi wa fedha wa Jahazi, Seif Magwaru amesema katika onyesho hilo mwimbaji mkongwe Bi Mwanaidi Shaaban atamsindikiza Mzee Yussuf na wimbo wake "Nitakufa kwa ahadi"Aidha Magwaru ameongeza kuwa onyesho la pili la Mzee Yussuf litakuwa Jumatatu 14/2/2011 siku ya wapendanao katika ukumbi wa Bulyaga, Temeke."Mambo mengi yamezungumzwa juu ya afya ya Mzee Yussuf ikiwemo kuzushiwa kifo, lakini hakuna haja ya kuandikia mate, mashabiki waje kwa wingi katika maonyesho hayo mawili washuhudie wenyewe maendeleo ya mwimbaji wao kipenzi" alisema Magwaru.FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :