News
Loading...

Hitma ya Marehemu Abuu Semhando leo!Mkurugenzi wa kampuni ya ASET Asha Baraka 
akizungumza na vyombo vya habari kulia ni
 marehemu Abuu Semhando na Luiza Mbutu.
  

Kampuni ya African Stars Entertanment (ASET) leo hii itamsomea hitma marehemu Abuu Semhando aliyefariki siku ya tarehe 18/12/2010 kwa ajali ya barabarani maeneo ya Africana jijini Dar es Salaam, baada gari aina ya Benz kuigonga pikipiki yake kwa nyuma, marehemu alithibitishwa kufariki eneo la tukio kabla hajafikishwa hospitalini.


James Kibosho aliusiwa na marehemu
atafute mpiga dramu wa kumsiadia.
Kifo cha Abuu Semhando ni pigo kubwa kwa bendi ya Twanga pepeta na tasnia nzima ya sanaa ya muziki wa dansi na muziki kwa ujumla nchini Tanzania. Hitma hiyo itafanyika leo saa 7 mchana katika ofisi za ASET Kinondoni vijana nyuma ya Mango garden karibu na Kinyaia's Pub. 

  
Siku chache kabla ya kifo chake marehemu alimwambia James Kibosho(mpiga dramu chipukizi) kuwa atafute mpiga dramu mwingine wa kumsaidia kwa kuwa yeye (marehemu) anakwenda likizo na hata akirudi asingepiga tena dramu, kwa kifupi ni kama alikijua kifo chake kimemkaribia kwani tunatanabahishwa kuwa pia alielezea kuwa amelipa madeni kadhaa aliyokuwa nayo.

Marehemu Abuu Semhando ameacha watoto kumi na moja toka kwa wake tofauti, ila habari za ndani zinaeleza kuwa miezi mitano iliyopita alioa mke mwingine ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga wilayani Muheza, marehemu Abuu Semhando pia alikuwa mwenyeji wa kijiji cha Kibanda wilaya ya Muheza mkoani Tanga ambako ndipo alipozikwa.
Mungu ilaze pema peponi roho ya kaka yetu mpendwa Abuu Semhando.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :