News
Loading...

Kesi ya mauaji Swetu Fundikira: Upande wa utetezi wafunga ushahidi


Ndugu wa marehemu wakitoka mahakamani 
Kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira inayowakabili maaskari jeshi sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi ambao wanadaiwa siku ya Jumamosi tarehe 23/Jan/2010 walimpiga bila huruma Swetu Fundikira katika maeneo ya Kinondoni Br ya Mwinjuma na Kawawa mpaka kusababisha kifo chake. Iliendelea tena leo asubuhi kwa mshtakiwa namba tatu kutoa ushahidi wake. Akionesha kutokuwa na uhakika na yale ayasemayo Mohamed aliiambia mahakama kuwa marehemu Swetu alipigwa na wananchi wenye hasira katika makutano ya Br ya Mwinjuma na Kawawa huko Kinondoni jijini baada ya wao kupiga kelele za wanatuua wanatuua. Ndipo watu hao wakampiga Swetu na kumchania nguo na kumuacha uchi. Wakili wa serikali akamuuliza "Mlipokuwa mnampeleka polisi marehemu kama mlivyodai kwa nini hamkuchukua japo watu wawili toka eneo la tukio ili muende nao polisi kama mashahidi wenu wa kuelezea kilichotokea hapo? Mohamed akajibu "Hakuna mtu aliyetaka kufutana na sisi kwenda polisi. Katika hatua nyingine mshtakiwa huyo wa tatu alidai kuwa walipokuwa katika gari Koplo Ali Ngumbe aliendesha gari Sajent Rhoda Robert alikaa mbele kushoto kwa dereva na yeye Mohamed na marehemu walikaa nyuma huku yeye akikaa nyuma ya dereva na marehemu nyuma ya Rhoda. Aliieleza mahakama kuwa marehemu aliyekuwa kama amepoteza fahamu wakati wakitoka Kinondoni alizinduka walipofika maeneo ya Upanga karibu na jamatini akafungua mlango na kuruka ambapo yeye aliwahi kumwambia dereva (koplo Ali) "funga breki anaruka huyu" ambapo dereva alifunga breki kwa ghafla na gari lilipokaribia kusimama marehemu akaruka na kuangukia kichwa kisha akainuka na kuanza kukimbia kama aliyepata kiwewe lakini hakufika mbali akakamatwa na security guard wawili wa kampuni ambayo hakuweza kuitambua. Akaendelea kusema "tulipofika pale mimi na mshtakiwa namba moja Rhoda tukawaambia wamuache kwani tunampeleka central police station, wakasema kwa nini msimpeleke Selander Bridge pia pana kituo cha polisi? Tukawajibu hatukujua kama pana kituo cha polisi pale kwa sababu sisi si wenyeji maeneo hayo. Mara ikapita taxi ikasimama kujua pana tatizo gani ndio tukamwambia nenda Selander Bridge polisi katuitie polisi tuna mtuhumiwa tunataka kumpeleka hapo. Alimaliza Mohamed. Baada ya kumhoji historia yake ya kazi Mshtakiwa wa namba tatu Jaji Mruke alimuuliza  "Wewe ni askari mahiri, ndio maana hata kazini kwako wamekupa cheo kama Bwana kilimo msaidizi, si ndivyo? Akajibu "Ndio! Sasa kwa nini wewe ulikaa na marehemu peke yako kule nyuma wakati kwenye gari milikuwa askari watatu, na kwa nini hukumuita Mshtakiwa namba moja mkae wote nyuma ili kumdhibiti marehemu iwapo angeleta matatizo? Mshtakiwa wa tatu akajibu " Kwa hali aliyokuwa na marehemu na tekiniki zangu niliona hakukuwa na haja ya sisi kukaa wawili kule nyuma" Jaji Mruke akauliza tena "Je unaonaje tukisema wewe ndiye unayepaswa kubeba jukumu la yote ya yaliyotokea kule nyuma? Hapana Mh jaji! Alijibu Mshtakiwa wa tatu, Jaji Mruke akaongeza kama wenzio walikuamini wewe kumdhibiti marehemu na ukashindwa mpaka akaruka toka gari kwa nini wewe usibebe jukumu hilo? Mohamed alionekana kuchanganyikiwa kwa maneno yale ya jaji. Baadae Jaji huyo mwanamama makini alikubaliana na ombi la kambi ya utetezi kuwa kesi hiyo iahirishwe mpaka kesho ambapo mawakili wa pande zote watatoa majumuisho yao na kisha Mahakama itaeleza kama imewapata watuhumiwa na hatia ya kumua Swet Fundikira kwa makusudi na kisha kupanga siku ya kutoa hukumu.

Mawakili wa utetezi kabla usikilizwaji kuanza.

Mwendesha mashtaka PP Katto Ishengoma na Maushi

Baadhi ya waandishi wa habari na ndugu wa marehemu wakiwa mahakani.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :