Jana ijumaa Jaji Mruke wa Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam aliahirisha kusikilizwa kwa kesi ya mauaji inayowakabili askari jeshi watatu Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashid ambao ni ndugu wa damu, wanadaiwa mnamo tarehe 23/01/2010 katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara za Mwinjuma na Kawawa kwa makusudi walimuua Swetu Fundikira. Washtakiwa wote watatu wamekana shitaka mara zote waliposomewa.Washtakiwa wamekuwa wakidai marehemu alipigwa na pengine kusababishiwa kifo na wananchi wenye hasira pale Kinondoni. Dai ambalo lilipelekea Jaji Mruke amuulize swali mshtakiwa namba tatu alipokuwa akitoa ushahidi wake hapo juzi. Jaji Mruke alisema. Mshtakiwa namba tatu wewe na mshtakiwa namba mbili mmesiambia mahakama mnaishi airport na mshtakiwa namba moja Msasani huku marehemu alikuwa akiishi Kinondoni, katika hali ya kawaida nyinyi mkipiga kelele ya kuomba msaada watu wakajaa wale watu watampiga nani? Yule wa Kinondoni au nyinyi ambao hamjukani pale? Kesi itaendelea jumatatu ambapo mahakama itatoa uamuzi kama washtakiwa wamepatikana na hatia ama la, na kisha itapangwa tarehe ya Judgement.
Kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira: Mawakili wamaliza kazi zao

0 comments :
Post a Comment