News
Loading...

Wazee wa baraza wafanya kioja kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira



Wazee wa baraza Ali Kampea kulia, Bibi Johari na MzeeRaha Saidi
Jana katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam wazee wa baraza katika kesi ya Swetu Fundikira waliushangaza umma uliohudhuria kesi hiyo (nafikiri hata na ndugu wa washtakiwa hawakutegemea kile walichosikia) baada ya wote watatu kudai kuwa washtakiwa waachiwe huru kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa wao walimuua Swetu Fundikira. Aliyetoa kali kabisa ni Mzee Raha Saidi aliyedai polisi wamewabambikia kesi washtakiwa ki ujanja ujanja. Mzee mwingine Ali Kampea alidai kifo cha marehemu ni ajali tu kwani alianguka ndipo akaumia kichwani na kupeleka kifo chake. Bibi Johari yeye alidai kuwa yeye haoni kama washtakiwa walikuwa na nia mbaya na hatimaye kumuua Swetu Fundikira bali washtakiwa ni watu wazuri na nia yao ilikuwa ni kumpeleka polisi tu na si vinginevyo hivyo yeye anaona hawana hatia.

Kabla ya kuwapa nafasi ya kutoa maoni yao Jaji Mruke aliwasomea vipengele vinavyotakiwa kuangaliwa ili kuweza kutoa maoni navyo kama ifuatavyo:
Baada ya Mhe. Jaji kutoa majumuisho yake alisema; ili kesi ya mauaji iwepo na mshitakiwa athibitike ni lazima pawepo na mambo manne(4) muhimu

1.Ithibitike marehemu amefariki
2.Awe amekufa kifo kisicho cha kawaida (not natural death)
3.Ithibitike washitakiwa ndio waliosababisha kifo
4. Je, kulikua na NIA OVU?

Mheshimiwa jaji alisisitiza kuwa ni kweli aliyefariki alikua Swetu R. Fundikira au Swetu Fundikira kulingana na taarifa ya polisi na daktari.

Kifo cha Swetu hakikuwa cha kawaida kwa sababu alikutwa uchi (kifo cha dhulma au kifo cha kinyama) Swetu amekufa kutokana na majeraha ya kichwani yaliyo sababisha kuvuja kwa damu kwenye ubongo na kusababisha kifo hivyo hiki si kifo cha kawaida

Pia Roda Robert, Ally Ngumbe na Mohammed Ally ndio waliondoka na marehemu Swetu maeneo ya njia panda ya Mwinjuma na kawawa akiwa katika afya njema na ndio waliokutwa wakiwa na marehemu Swetu br. Ali Hasani Mwinyi eneo na Jamaat opposite na ofisi za TPDC kando ya barabara akiwa katika hali ya kutojitambua kwa hiyo hakuna mashaka kuwa wao ndio waliokuwa wanaojua kilichompata Swetu kabla ya kukutwa na mauti na wao (washitakiwa) walikua wanatakiwa kuthibitisha kilichompata Swetu. Na pia hapakua na shaka kuwa wao ndio walikua na Swetu kwani hata wao wenyewe wamethibitisha hilo bila kuacha shaka

Kuhusu nia ovu ni Mhe. Jaji alieleza kuwa ni dhahiri kutoka na ushahidi uliotolewa washitakiwa walikua na nia OVU kwani Rhoda anaishi maeneo ya msasani hivyo ni wazi kuwa alikua anapajua O'bay police station vyema lakini cha ajabu waliposema wanampeleka police ni wazi walitakiwa kumpeleka Oyster bay police lakini hawakufanya hivyo

Mheshimiwa Jaji baada ya kutoa ufafanuzi huo aliendelea kusema kuwa ilikutoa maamuzi ya kesi juu ya nia OVU ni muhimu kuzingatia mambo manne(4) muhimu yafuatayo:
1. Kuangalia aina ya silaha iliyotumika
2. Kuangalia nguvu iliyotumika katika tukio
3. Kuangalia aina/kiwango na eneo yalipo majeraha
4. Kuangalia tabia ya mshitakiwa kabla /baada yatukio
(maneno yake kabla/ baada ya tukio)

Silaha iliyotumika ni kwamba alipigwa na kitu kisicho na ncha kwa kurudiarudia
tena kwa force kubwa kwa kiwango sawa

Sehemu aliyopigwa ilikua kichwani kwa mujibu wa Dr. hii ikiwa na maana kuwa walidhamiria ndio maana walichagua sehemu ya kichwani na si sehemu nyingine

kuhusu tabia ya washitakiwa ni kwamba kwa nyakati zote hawakuonyesha hali ya ubinadamu kwa marehemu Swetu R. Fundikira kwani hata pale walipokutwa nae alikua uchi na hata walipogundua kuwa alikua muhimbili kwa maelezo yao mbele ya mahakama walisema kuwa walikwenda Muhimbili kwa kulazimishwa na polisi na wala si kwa hiari yao.

Kesi hiyo itatolewa hukumu na mahakama tarehe 30/10/2012

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :