News
Loading...

Kesi ya Swetu Fundikira: Watuhumiwa atoa ushahidi wao


Baada ya jana upande wa mashataka kufunga ushahidi jana, leo Jaji Zainabu Mruke ametoa uamuzi kuwa upande wa mashtaka umeweza kusimamisha kesi hivyo basi washtakiwa watatakiwa kujitetea wenyewe kwa kuwa hawakuleta mashahidi. Jaji Mruke alisema "Kwa kuwa upande wa mashtaka umeweza kuleta mashahidi sita na wametoa ushahidi mzito, na upande wa utetezi umeshindwa kuleta mashahidi hivyo basi mahakama hii imeamua kufanya uamuzi mdogo ambao ni kama ifuatavyo, washtakiwa wote watatu watajitetea wenyewe kwa kuwa hawana mashahidi zaidi yao wenyewe.Hivyo basi mshtakiwa wa kwanza atapanda katika kizimba cha shahidi na kutoa ushahidi wake.

Baadhi ya ndugu wa marehemu nje ya mahakama
Sajent Rhoda Robert alipanda kizimbani na kuanza kujibu maswali ambapo majibu yake mengi yalitofautiana na maelezo yake aliyoyatoa baada ya kuhojiwa na polisi wa kituo cha Oysterbay. Kwa mfano alipoulizwa na kwa nini marehemu alikuwa uchi walipokutwa nae? wakati mashahidi wa mashtaka walisema walipoondoka naye toka br ya Mwinjuma na Kawawa alikuwa na nguo zake na katika hali nzuri? Yeye alijibu kuwa tangu walipomchukua pale hakuwa na nguo baada ya nguo zake kuchanwa na wananchi wenye hasira pale Br ya Mwinjuma na Kawawa. Kitu ambacho katika maelezo yake Koplo Eustace alipowauliza kwa nini marehemu yupo uchi? sajent Rhoda alijibu nguo zake zipo katika gari na Koplo Eustace alipoenda katika gari alizikuta nguo za marehemu humo. Pia jaji Mruke alimuuliza Sajent Rhoda "siku ya tarehe 23 ulienda Muhimbili kumuona marehemu, je ulienda kwa hiari yako au kwa sababu ulitakiwa kwenda huko? Rhoda akajibu "Mimi sikutaka kwenda ila nilitakiwa niende kumtambua mtuhumiwa wetu" Jaji Mruke akamuuliza tena " Sasa Rhoda kama ulitaka kumpeleka polisi marehemu kwa nia nzuri tu kwa nini katika hali ya kibinadamu hukutaka kwenda muona marehemu na ulisikia alikuwa na hali mbaya ICU? Rhoda akajibu "Ah mimi sikutaka tu" Kesi itaendelea kesho kwa mshtakiwa wa tatu Mohamed Rashid kutoa ushahidi wake.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :