News
Loading...

Usafiri huu ni rahisi lakini ni hatari sana!


Nikiwa bajajini.
Jana nilishuhudia kwa macho yangu (England wanasema FIRST HAND) jinsi madereva wa Bajaj wanavyohatarisha maisha yao na ya wateja wao na si ajabu kuona ajali zinazohusisha tuku tuku hizo zinazidi kuongezeka. Yaani huwezi kuamini jinsi wanavyoendesha kwa fujo kwa ghafla nilifikiri dereva huyo kapandwa na shetani au kawehuka yaani nilikuwa roho mkononi.Nilitokea kuipanda Bajaj hiyo baada ya kuzimikiwa na gari, na kitu cha kwanza kufikiri ilikuwa labda imeisha mafuta ndipo nikaisimamisha na kumtaka anipeleke kituo cha kuuzia mafuta na kurudi pale ilipo gari, na hasa hapakuwa mbali ilanilitaka kufanya mambo kwa uharaka zaidi.Na nikiwa napelekwa kituo cha mafuta nikawaza na kujiuliza kulikoni bado Bajaj hizi zina wateja kem kem, sikupata jibu? Ndio maana niliporudishwa pale nilipoacha gari nikiwa salama nikamwambia dereva tupige picha. Jamani kupanda Bajaj ni kujihatarishia maisha, namuomba Mungu asiniweke katika hali ambapo nitalazimika kupanda tena Bajaj. Nashauri Mamlaka husika zifanye kitu kuhusu hawa madereva wa Bajaj, wasiachiwe waendelee kuvunja kila sheria ya barabarani.FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :