News
Loading...

Huu ni uchawi au ugonjwa tu? True Story!


Hiki si kipara kinachipua, La hasha haya ni matunda
 ya kudai haki kwa baba mwenye nyumba.
Hiki ni kichwa cha msichana mrembo ambaye anaishi maeneo ya Kinondoni kwa sasa anayejulikana kwa jina la Jay ili kuhifadhi jina lake halisi. Na hiki ukionacho katika picha juu ni kichwa chake kilichonyolewa kimazingara na ni matunda ya yeye kubishana na baba mwenye nyumba wa nyumba aliyokua akikaa maeneo ya Kinondoni B block 42/ au FAO. Binti huyo mrembo alikaa katika nyumba hiyo kwa muda wa miezi nane. Ambapo yeye amekuwa mwajiriwa wa taasisi fulani maarufu hapa jijini kama mcheza show na mwimbaji. Lakini kwa bahati mbaya tena bila yeye kujua kwa kipindi chote alichokaa pale amekuwa akimuudhi baba mwenye nyumba wake kwa mazoea yake ya kurudi usiku mwingi takriban kila siku na hii ilitokana na asili ya kazi yake. Siku moja mida ya asubuhi paliwekwa ndoo za taka mbele ya nyumba aliyokuwa akikaa binti huyo baba mwenye nyumba akaziona taka zile, kwa jinsi alivyoamua yeye aliona taka hizo ziliwekwa hapo na binti Mrembo Jay bila kumpa nafasi ya kukiri au kukanusha dai hilo. Kwa kutumia busara zake zote Mzee yule akaona ni bora amwachie taka zile Jay nje ya mlango wa chumba chake . Yaani akiamka na kuzikuta pale nje ya mlango wake ataziondosha na kwenda zitupa. 
Muda ukawadia Jay akaamka na hata alipoziona taka zile hakuzitoa taka zile kwa muda wa siku mbili hivi. Siku ya tatu ndipo Mzee yule anamuuliza Jay Kwamba kwa nini bado taka zile bado zipo pale?Jay akamjibu hafahamu kwa nini na nani aliziweka hapo. Kwa ghafla wanajibishana kwa maneno machafu huku mama wa Jay akiwepo. mwisho wa ubishi ni pale Mzee yule alipomaliza kuongea Jay kwa kusema" wewe si unajifanya mjeuri? basi mimi nitakuonyesha wewe. Baada ya usiku huo kupita ndipo kesho yake Jay anakwenda saloon kuweka less wig ndio anagundua kuwa alifanyiwa kitu mbaya.Kwa mujibu wake Jay yeye alitaka kuweka less wig ndipo wahudumu wa saloon wakamwambia kuwa ana uwazi mkubwa kichwani na wakamuwekea vioo ili naye ajione. Tangu siku hiyo ametumia dawa za aina na aina lakini nywele hazioti. Sasa mdau swali langu mimi je wewe unafikiri huo ni uchawi au ni Kudra za Mwenyezi Mungu? Tafadhali tuma maoni chini ya makala hii.

 Tafadhali tuma maoni chini ya makala uisomayo 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :