News
Loading...

Obama Ivory Coast vipi?


Machafuko Abidjan
Yaani hawa mabeberu hawana aibu wala haya, wamekaa kimya tu wakati Bagbo anang'ngania madaraka na kuua raia wasio na hatia kule Cote de voire pana watu 450,000 wamekimbia makazi yao, na jana tu wameuawa wanawake nane huku wakiwa hawana silaha zaidi ya sufuria na makarai na miili yao imeachwa ikiliwa na mbwa barabarani Na hivi nikiandika hii makala pamepigwa bomu sokoni huko Abidjan na watu wasiopungua 30 wamekufa. Sasa marekani na vibaraka wake Uk, France na Germany wanasubiri nini kwenda mtoa madarakani Bagbo?Au kwa kuwa hakuna mafuta pale? Najiuliza Mwalimu Nyerere angekuwepo sijui angesemaje maana najua hakuwapenda kabisa watu wanafiki na MABEBERU kama hawa Uk, France na Germany na kibosile wao Mmarekani wao wamemkomalia Ghadaffi kwa kuwa Libya pana mafuta na si kutaka demokrasi kama wanavyodai, tunajua walipeleka Demokrasi IRAQ na mpaka leo ni nchi ya amani. Nikiwa natoka katika kabila la Wanyamwezi naona aibu Mmarekani kuitwa Mnyamwezi, kwa kuwa Mnyamwezi ni mstaarabu!
Obama anataka nini zaidi kitokee zaidi ya hiki?
Kakosa nini mtoto huyu?

Maiti, chakula cha mbwa.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

HAHAHA.kweli noma..umeona mbali Mkuu wa kambi ya ukweli duniani.bora wangekuchagua uwe mbunge wa viti maalum wewe kuliko kuchagua madems,kwa kuwa kuna siri hapo uchaguzi wao ,we unastahiki sana uwe kiongozi bora kwa jamii mwana wa kutobora...MDAU BELFAST

Anonymous said...

Duuh umenigusa mwake MPWAA.
mdau DEN HAAG