News
Loading...

NEC hii iliyofeli kwa miaka 10 kwa nini bado ipo?


Hongera sana kwa dosari zilizojitokea katika uchaguzi.

Nchi hii inasikitisha sana, ile tume ya uchaguzi iliyokuwa ikishindwa kufanya kazi ipasavyo kwa miaka zaidi ya kumi na tano kuanzia mwaka 2000 mpaka katika uchaguzi uliopita, bado Mh Rais J Kikwete ameishilikilia kubaki kuindesha tume hiyo pamoja na kuwa na dosari zisizo kifani katika utendaji wake. Unafikia wakati unajiuliza dosari hizo zinampendeza Mh Rais ndio maana haoni sababu ya kuifukuza kazi tume hiyo? Kwa maana ya kuwa dosari hizo zinakinufaisha chama tawala? Bila shaka uchaguzi mdogo wa Igunga utasimamiwa na Tume hiyo iliyo chini ya jaji mstaafu Lewis Makame lakini natumai hatutokuwa na tume hiyo bebwa ifikapo 2015. Uchguzi mdogo wa Igunga umepangwa kufanyika Oktoba 2 mwaka huu.

Jaji Mstaafu Lewis Makame- Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

4 comments :

tz biashara said...

Mkala hongera kwa kuipamba Blog na inapendeza.
Siasa ya kwetu haina mwelekeo naona mauzauza tuna ndio maana tunaishi kwenye kiza.Sikufichi Mkala siiamini serikali yeyote hapa japo mabadiliko tunayataka.Na kama tunataka mabadiliko basi sio kwa viongozi tu bali mpaka sisi wananchi.Kwa sababu nchi haijengwi na viongozitu bali ni wananchi ndio wanaoijenga nchi.Na kama wananchi wataonyesha msimamo mkali na kuwa makini basi viongozi wataogopa na kujaribu kufanya kazi zao kwa umakini.Msimamo mkali ni pamoja na upigaji kura.Ikiwa tumeona CCM haikuzaa matunda basi tujaribu kubadili chama na kama chama kingine hakijafanikisha vilevile kipigwe na chini mpaka kieleweke.Hapo lazima kila kiongozi atakuwa mkali na kazi yake kwa kuogopa kutochaguliwatena.Lazima tuwe na mapenzi na nchi kwa kuangalia umuhimu wa nchi na wananchi na sio kuangalia dini au kabila hapo watanzania hatutafanikisha ndoto yoyote.Tunatakiwa tuungane na kutoa tofauti zetu tulizonazo ili kuwaonyesha viongozi hakuna tunahasira na nchi yetu.

Mkala Fun said...

Nakubaliana na wewe kabisa, tuiondoshe CCM madarakani tuweke wapinzani, miaka mitano inatosha sana kujua utendaji wa taaasisi yeyota, nasi tutakua tumejua utendaji wa wa wapinzani ifikapo 2020 au kabla ya hapo then tunakua na maamuzi ya kufanya 2015. Mungu ibarika Tanzania!

Mkala Fun said...

Tutakua na maamuzi tuwaache wapinzani mdarakani au tuwapige chini ifikapo 2025

tz biashara said...

Ila Mkala sikiamini chama cha CHADEMA kinatishia amani.Chama chao kitakuwa zaidi ya CCM hivyo kwa watanzania waangalie sana ktk kuchagua chama chenye dhamiria ya maslahi ya Taifa na sidhani kama kina Mbowe na Slaa wanayo hiyo dhamiria.Hebu tafuta mzalendo.net halafu ktk page yao ukishuka chini pana video naomba ukipata nafasi uzipitie tafadhali.Halafu nifahamishe hata kwa email yangu umezionaje ni muhimu sana.