News
Loading...

Miaka 50 ya Uhuru itakayoadhimishwa na ukosefu wa UMEME, MAJI NA MAFUTA


Wapendwa wadau kama mjuavyo mwaka huu tuta adhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu Tanzania Bara, lakini katika mwaka huu kumekuwa na matatizo mengi katika nchi hii ikiwemo tatizo sugu la ukosefu wa umeme, mfumuko wa bei, ukosefu wa maji ya uhakika na sasa ukosefu wa mafuta ya kuendeshea gari na yale ya taa. Mara ya tatizo hili kujitokeza iliichukua serikali siku tatu kutoa kauli  iliyotolewa na waziri mkuu Mh Pinda bungeni akisema "serikali haiwezi kuingilia utendaji wa EWURA iliyopewa dhamana ya kusimamia bei za maji na nishati" Mimi binafsi nilishangazwa na jibu hilo la waziri mkuu akijibu swali la Mh Freeman Mbowe aliyetaka kujua nini msimamo wa serikali baada ya kampuni kadhaa za uuzaji wa mafuta ya reja reja (Gas stations) kugomea bei elekezi iliyotolewa na EWURA na kusababisha upungufu wa nishati hiyo muhimu karibu nchi nzima. Ikiwa imeingia siku ya nane jana ya ukosefu wa nishati hiyo ndio EWURA wametoa tamko kuwa huduma ya mafuta irudi katika hali ya kawaida within 24 hours au wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. Jana ilifikia baadhi ya watu waliohojiwa na Runinga kadhaa kuuliza ilipo wapi serikali yao na wengine walikwenda mbali zaidi na kuhoji kuwa nchi hii ina Rais? na kama yupo ni ni vipi aachie watu kadhaa wasimamishe uchumi wa nchi nzima? Sio siri, mimi pia nahoji tuna serikali inayofanya kazi kweli?

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :