News
Loading...

Mdau tzbiashara ataka wa Tanzania wabadilike!


Mkala hongera kwa kuipamba Blog na inapendeza.
Siasa ya kwetu haina mwelekeo naona mauzauza tuna ndio maana tunaishi kwenye kiza.Sikufichi Mkala siiamini serikali yeyote hapa japo mabadiliko tunayataka.Na kama tunataka mabadiliko basi sio kwa viongozi tu bali mpaka sisi wananchi.Kwa sababu nchi haijengwi na viongozitu bali ni wananchi ndio wanaoijenga nchi.Na kama wananchi wataonyesha msimamo mkali na kuwa makini basi viongozi wataogopa na kujaribu kufanya kazi zao kwa umakini.Msimamo mkali ni pamoja na upigaji kura. Ikiwa tumeona CCM haikuzaa matunda basi tujaribu kubadili chama na kama chama kingine hakijafanikisha vilevile kipigwe na chini mpaka kieleweke. Hapo lazima kila kiongozi atakuwa mkali na kazi yake kwa kuogopa kutochaguliwa tena. Lazima tuwe na mapenzi na nchi kwa kuangalia umuhimu wa nchi na wananchi na sio kuangalia dini au kabila hapo watanzania hatutafanikisha ndoto yoyote. Tunatakiwa tuungane na kutoa tofauti zetu tulizonazo ili kuwaonyesha viongozi kuwa tuna uchungu na nchi yetu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :