News
Loading...

Usingizi gani huu?


Mtoto Neysha akinyonya juice maarufu kama kijoti lakini pia akijisinzilia, taabu ya nini bwana starehe mbili ndio mwake.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

8 comments :

Subi Nukta said...

ha ha ha haaa, safi sana!
(hivi bw. Kero Nyingi, ule mwendelezo wa yule bwana aliyenyimwa mke hadi atakapojiweza umeuweka? Nimekuwa nausubiri)

Mkala26 said...
This comment has been removed by the author.
Mkala26 said...

Yule bwana aliniambia bi harusi bado anataka kuolewa naye na kuwa alienda kupacheki home mwenyewe na akaparidhia. Sasa sijajua zaidi. Ndio maana sikuweka tena picha za nyumbani kwake. Lakini ni pazuri tu, I wud be proud to have makazi kama yale.

Subi Nukta said...

Mkala, shukran kwa kwa majibu.
Kama ulipaona na ulipapenda, basi sina shaka ni kiwewe tu kiliipitia familia ile, Mola awape maono safi zaidi.

Mkala26 said...

Jana usiku nilimuona Najib nikamuuliza tena kuhusu ile sakata ya bi harusi, akasema wazazi wake wamekuwa wakimnyng'anya simu na kujifanya ni yeye wakichati na Najib. Akisema mimi sikutaki na mengi mabaya huku akimtuhumu kuwa na wanawake wengi lakini hatimae binti anampigia na kumwambia hakuwa yeye akichati naye bali ni ami yake. Lakini Najib kaamua basi kisicho rizki hakiliki.

Subi Nukta said...

Mkala, alichoamua Najib kwa sasa naafiki kuwa ni sahihi kutokana na hali halisi ya mambo. Kulazimisha hatima yake huwa heshi vizuri. Ya nini kuishi maisha ya mashaka na kero tangu siku ya kwanza watapapooana wakati imeshaanza kuonekana ishara kuwa wakwe watatia nyongo chakula kisilike? Aache tu. Huenda anajiepusha na shari kubwa.
Asante Mkala kwa 'update'. Nimejifunza katika kisa hiki na ni nani ajuaye, huenda kikawa jawabu kwa wengine wanaopitia njia izo hizo na pia funzo kwa wanaokwenda kuchumbia/chumbiwa.

Mkala26 said...

Ni kweli Subi, yaweza kuwa funzo kwa wengine.Lakini inashangaza kuwa bado kuna familia zina utamaduni wa kuchagulia wachumba watoto wao, nafikiri ni aina fulani ya utumwa, imagine wewe umeozwa kwa mtu ambaye hukumpenda lakini ukaishi nae mpaka mkazaa watoto, utakuwa unajisikiaje moyoni huku ukiwa unamjua unayempenda wewe na ambaye ndiye ungependa kumzalia? Ni kinyume na haki za binadam kabisa, ninavyofikiri mimi.

Subi Nukta said...

Umesema vyema Mkala.
Siafiki tabia ya wazazi kuingilia au kuchagulia watoto wao (wakike au kiume) wenza wa kuishi nao. Ni maisha ya milele. Afadhali wakuongoze, wakuambie uzoefu wako, kwa kuwa u mtu mzima mwenye akili timamu ya kufanya maamuzi, basi wakuache uamue utakalo wewe na utakalolisimamia ili mbeleni usijelaumu wazazi kwa kutaka ufanye wayatakao wao badala ya ulitakalo wewe na mwenza wako.

Enzi za kulazimishiana wenza si hizi jamani, si dharau au kujifanya kwenda na wakati, ila ni kuheshimu uamuzi binafsi wa mtu aliye binadamu kamili mwenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi au potofu kwa utashi wake.