News
Loading...

Kesi ya Swetu bado kitendawili


Mtoto Sivuno Swetu akifurahia siku ya kuzaliwa

Kesi ya mauaji ya inayowakabili askari jeshi (JKT) watatu wanaotuhumiwa kumuua Swetu Fundikira kwa kumpiga mara nyingi kichwani kiasi cha kupelekea mvujo wa damu katika ubongo wake na kusababisha kifo chake saa 24 baadae. Watuhumiwa hao ni Sajin Rhoda Robert 46, Ally Ngumbe 38 na Mohamed Ally Ngumbe 28 ambao ni ndugu bado kusikilizwa kwake ni kitendawili. Pamoja na kuwa upelelezi ulikamilika tangu mwezi Januari 2011 na jalada la kesi hiyo kuwa imepita idara zote husika na hatimaye kufika Mahakama Kuu ambapo ndio yenye uwezo wa kusikiliza na kutoa hukumu ya kesi za mauaji. Imebainika tararatibu za mahakama kuu ni kuwa kesi hiyo na nyingine zinazosubiri kusikilizwa ni mpaka zikaliwe kikao na zipitishwe na kupatiwa bajeti ya kusikilizwa. Kikao hicho hufanyika mwezi wa sita, na kwa jinsi nilivyofahamishwa ni kuwa si kesi zote zitapitishwa kusikilizwa ni baadhi tu. Napenda kufikiri kuwa kesi ya Swetu Fundikira ina mvuto wa hisia kwa jamii (Public interest) hivyo sina shaka itakuwa moja kati ya kesi zitakazopita kusikilizwa katika mchujo huo hapo june 2011.

Pichani Sivuno Swetu Fundikira(1) hana hili wala lile ni mwenye furaha kubwa lakini baba yake alifariki miezi sita kabla yeye kuuona ulimwengu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :