News
Loading...

Udadisi wa kifo cha Osama unaponiponza kutuhumiwa kwa udini!


Mimi na Rugeh Mutahaba wa clouds Fm.
Mpendwa mdau kama unakumbuka siku kadhaa nyuma niliandika makala yenye kichwa "Kwa jinsi tunavyoijua mentallity ya Waarabu" humo nimeeleza wasi wasi wangu juu ya jinsi America inavyoeleza ilimuua Osama Bin Laden, kwa jinsi Marekani ilivyokuwa ikimtafuta kwa vyovyote Bin Laden angekua na silaha kila pahala alipokaa ndani ya kasri lake mjini Abottabad pengine hata msalani. Silaha hiyo si kwa kuwadhuru maadui zake, la hasha, ya kujitolea uhai yeye mara atapokuwa anakaribia kukamatwa akiwa hai.  Na hatimae nilisema" labda White House iieleze dunia ni jinsi gani Osama alikufa" Mpendwa mdau ukisoma makala hiyo haina hata mstari mmoja unaokataa kuwa Osama hajafa bali makala hiyo inahoji jinsi gani alivyokufa tu. Nanukuu comment ya anonymous mdau kama alivoniandikia neno baada ya neno na spelling alizotumia katika makala hiyo "Kaka huo ushabiki tu, Osamba is dead, walishamua sasa wewe unataka kubishana na mtoto wake au mkewe? Au unataka kubishana na kundi lake lenyewe walio confirmed kuwa amekufa......... huo ni ushabiki wako wa udini tu. Acheni hayo" Mwisho wa kumnukuu Anonymous mdau. Ndugu mdau ukiingia katika makala hiyo na ukasoma comment zake utaelewa tatizo lipo wapi ila si kwangu na sitoingia katika mjadala juu ya dini. Mwl Nyerere alipata kusema dhambi ya ubaguzi ni kubwa sana, ukimbagua mtu kwa dini yake, pia utafikia kumbagua kwa dhehebu kisha utambagua kwa kabila, rangi, mahala anapoishi na pengine kasoma shule gani, alimradi ubaguzi hauna kikomo na tunapaswa kuugopa kama Ukoma.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

6 comments :

Anonymous said...

Nadhani mdau alikuwa sahihi, nyinyi waislamu kila kitu cha Osama mnatetea hata dini yenu haisemi hivyo, mnachukulia Marekani ni kama taifa la Kikristu.

Anonymous said...

Wewe ni mdini tu...sasa unajitetea nini?

Mkala Fun said...

Wadau wapendwa nachukua nafasi hii kuufunga mjadala wa kifo cha Osama it seems i m in a no win situation whatever point i make is useless, some of you who have gone too far to even say "Nyinyi waislamu". I just think for the unity of this country lets shelve this Osamamania. Nawashukuru nyote kwa michango. Lets move on Guys!

Anonymous said...

Mimi nadhani hapa sijui kama ni ubaguzi wa dini au ni wa rangi.Kwa sababu hicho kichwa cha habari ulivokiweka sidhani kama ni sahihi.Ukitoa hilo neno mwarabu halafu weka mswahili sijui kama ungefurahika kaka.Ukiwa ni mwana BLOG nadhani ni muhimu kujivua "gamba"kama unalo.Huyu Osama akifa au akiwa mzima hatuwezi kufaidika chochote wanaofaidika ni hao marekani.Na kama uisilamu, ni dini moja ambayo inaeleza waziwazi kuhusu uasi wa kuua au kutesa binaadamu hata kama sio muisilamu mwenzio basi mtu huyu atakuwa na fungu baya mpaka kiyama.Kwahiyo kaka msiwe mnatumia njia za kupotosha dini au kabila za watu ni muhimu mjifunze kwa undani na muyajue ukweli wake.Tutumie haki ambayo itafafanua mengi na kufaidisha wengi.

Mkala Fun said...

Nashukuru kwa maoni yako mdau, ukisoma juu maoni yako kuna maoni yangu, nikiomba tuufunge mjadala huu humu bloguni, kwa kuwa it has been blown out out of porpotion. Nilichouliza katika makala kuu ni kuwa je? Osama alikaa akiwasubiri wamarekani wamvamie chumbani mwake bila kujaribu kujitoa uhai? Si kuwa nlisema hajafa! Kwa nini kila anaye comment analiruka hilo? Aliyetoa comment ya udini ni mmoja wa wadau. Ukisoma kila comment utagundua ukweli wa ninachdai. Nakuomba soma makala kuu na comments zote kisha uwasiliane nami humu 0754666620 tuwekane sawa. Na narudia tena kuwaomba wadau msitume comment juu ya Osama kwa kuwa mjadala kuhusu yeye niliufunga humu.Otherwise lets move on!

tz biashara said...

Hello!! Ruge Mutahaba..Kwanza nimefurahi umeingia ktk blog yangu ambayo najifunza kuitumia na wala sio mjuzi ila husband ndio ananisaidia jinsi ya kuandaa matokeo mbalimbali.Sasa kaka yangu nilijua ile ishu hujataka kuizungumzia tena na vilevile nafahamu jinsi gani hapo unapojisikia mtu anapokuja na jazba yake na kutokubaliana na maelezo yako.Ruge kaka yangu usichukie sana hayo ni mambo ya kawaida na wala sio wakumuekea kinyongo mtu.Unajua kila siku zinavokwenda mbele basi watu pia wanabadilika kwa kila jambo.Na ni vizuri kuyasoma ya duniani kwa umakini na kuyajua ukweli wake hasa ktk siasa ambayo tunadanganywa sana na bila kuona mafanikio yake.Kwa mimi nilikuelewa kwa jambo uliolielezea kuhusu Osama lakini labda ulikosea kuandika kichwa cha habari ambacho ni muhimu sana.Kichwa cha habari kilikuwa kina kasoro na jinsia ya kiubaguzi na pengine hayapo ktk moyo wako lakini hukujua ukitungie kipi ili uwape changamoto kwa wapenzi wako.Kawaida mimi hupenda kuingia blog tofauti na kuangalia habari na picha mbalimbali kutokana kwamba nipo mbali na nyumbani.Na pia navutiwa sana na blog yako kwa kuangalia jinsi mbeya ilivo kwasababu sijawahi kufika lakini nimekupenda kwakuwa ni GREEN ambayo inafurahisha.Lakini sikubaliani na kwamba walimuua huyo Osama kwa siku ile na ninaimani kama alikufa zamani japo sina uhakika wa 100%.Kwa hiyo usijali sana chukulia kama Mjengwa naona watu wanamzonga sana tu lakini hajali mradi anaendelea na maisha yake.Lakini pia ni changamoto ktk kujadiliana mambo mbalimbali na kupata kujua mengi.