Wenda kwa miguu hapa Tanzania wamekuwa hawathaminiwi kabisa, kwa mfano mtu anapotaka kuvuka barabara itambidi asubiri mpaka gari zitakapokwisha tu, hali ni tofauti katika nchi zilizoendelea kama England, mara utakapo kuvuka barabara unaenda ilipo sehemu maalum ya kuvukia panakuwa na traffic lights na kitufe katika picha kushoto ukikibonyeza huwaka taa nyekundu ambapo magari husimama na wenda kwa miguu huvuka bila taabu. Nafikiri hilo linaweza kufanyika hapa nchini ketu hasa Dar. Tena itawaondolea bugudha wenda kwa miguu ambao mara nyingi wamekuwa wakigongwa na magari wanapovuka mabarabara. Unaweza ukaambiwa taa zitawakaje wakati umeme ni wa mgao? Kuna Solar, basi na zitumike kufanikisha hili. Viongozi bora ni wale wanaojali wananchi wanaowaongoza na si vinginevyo.
Kibofyeo ambacho huwasha taa nyekundu. |
Hapa ni zebra cross Mlimani city. |
Hiki ni kivukio cha wenda kwa mguu Uk. |
0 comments :
Post a Comment