News
Loading...

Kama CHADEMA wanavunja sheria washitakiwe!


Afande nahodha Mh John Chiligati
Nimesoma malalamiko yaliyotolewa na afande Mh John Chiligati katika gazeti la Mwananchi la leo akivitaka vyombo vya dola vimchukulie hatua katibu mkuu wa CHADEMA Dk Wilbroad Slaa kwa kauli ambazo amekuwa akizitoa katika mikutano ya chama hicho huko kanda ya ziwa. Nashindwa kuelewa kwa nini Afande awe na shaka hivyo? Yaani vyombo vya dola vya Tanzania Havipigiwi vinacheza itakuwa vipigiwe si tutaona sarakasi hapa nchini! Yaani wanasubiri opportunity ijitokeze tu waanze kamata kamata, piga piga na ua ua! Labda afande hafahamu kuwa kuwa malalamiko yake yanazidi kuwajenga hawa mabwana wa CHADEMA, pia chama kikongwe hakina haja ya kuhofu, wamekuwa wakisema na kutamba kwa mazuri waliyowafanyia wa Tanzania sasa kama watu umewatendea mazuri una wasi wasi gani kuwa watakugeuka? Na kama CCM iliingia madarakani kwa ushindi mnono wa kura ina maana wananchi wana imani na chama hicho na serikali yake, tena hata miezi sita haijapita tangu wakichague. Hivyo mimi sioni ni vipi wananchi waigeuke serikali ya CCM na kuiondosha madarakani kimabavu kama Tunisia na Misri baada ya miezi minne tu kupita tangu kuipa ridhaa. Au vinginevyo hofu ya CCM inakuja labda kuna kosa wamewafanyia wananchi katika kipindi hiki cha mara baada ya uchaguzi, inawezekana ni mfumuko wa bei? au ni milipuko ya mabomu Gongo la Mboto? au ni malipo ya Dowans? Jibu silipati!  Nimemnukuu Afande Chiligati toka gazeti la Mwananchi akisema kuwa CCM haikutaka kulipa deni hilo la sh bilioni 94, lakini ninavyokumbuka Mh Sitta alipopinga lisilipwe Mh waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa sauti kubwa "LAZIMA LILIPWE" hata kama inatuuma kiasi gani, "TENA LILIPWE HARAKA IWEZEKANAVYO! Sijui aliposema hivyo alikuwa anawakilisha serikali ya chama gani labda tunahitaji kuwa na digrii moja kujua jibu ni lipi hapo!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments :

Anonymous said...

hawa chadema ni wahuni wataipeleka nchi kubaya

Anonymous said...

Hapo kwa Mh Pinda nipo hoi kabisa sipati jibu