News
Loading...

Kolo Toure hajafungiwa bado!


Toure kabla ya kusimamishwa.
Nimelazimika kukanusha kufungiwa kwa Toure kutokana na utata unaoanza kujitokeza katika vyombo vya habari vya Tanzania juu ya suala la aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Arsenal Kolo Toure. Leo hii nimeshuhudia kituo kimoja maaarufu cha televisheni inayosoma taarifa yake ya habari saa moja za usiku kikipotosha ukweli juu ya suala la kufungiwa Toure. Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha televisheni hiyo alisikika akisema kuwa Kolo Toure ambaye anachezea kilabu cha Manchester City cha England kafungiwa kucheza soka kwa miaka miwili baada ya kubainika kutumia madawa ya kulevya. Jambo ambalo si kweli kabisa sijui muandaaji wa kipindi hicho anapata wapi habari hizo lakini napenda kufikiri source yake ndiyo ile ile niitumiayo mimi na wengine wengi. Ukweli ni kuwa  
1.Kolo Toure amesimamishwa kujihusisha na chochote kinachohusiana na soka mpaka atakapofanyiwa vipimo vya pili baada ya mkojo wake kukutikana na chembe chembe zinazokatazwa na taasisi ya kuzuia utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu kwa wanamichezo(WADA) katika kipimo cha kwanza.
 
2.Kilichokutwa katika mkojo wake ni chembe chembe zilizopigwa marufuku na si madawa ya kulevya ya aina yeyote kama ilivyobainishwa na kituo hicho runinga kupitia kipindi chake cha michezo ambapo mwenyewe amelaumu diet.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Anonymous said...

asante sana kwa kutuelimisha