News
Loading...

Majungu ni kero sehemu za kazi!


Wapendwa wadau makala hii inatoka kwa mmoja wenu,
MAJUNGU NI KERO MAKAZINI
Napenda kuwahimiza wabongo waache unoko na wachape kazi kwani siku zote maneno hayajengi.
 
KERO YANGU NI HII HAPA
Nipo kituo kimoja cha redio x  natangaza vipindi vitatu vinavyonifanya niwe hewani siku 6 za wiki, nikiwa bado sijatimiza hata mwaka mmoja kituoni hapo nimefanikiwa kufanya kazi ambazo zimekubalika kwa wasikilizaji hadi kwa uongozi.
Lakini mafanikio yangu ambayo yalianza kuonekana tangu wiki ya kwanza yamefanya niandamwe na majungu ya kila aina.
Nimechafuliwa sana katika gazeti moja la udaku litokalo mara 2 kwa wiki ambalo lilinishambulia sana kupitia vyanzo ambavyo baadae niligundua vinatokea hapa hapa Radio X  pengine upeo wao mdogo uliwafanya waamini kuwa mtu anaweza kufukuzwa kazi kwa kashfa za kupandikiza magazetini.
Nashukuru kuwa Mungu ameanza kunilipia kwa baadhi ya wabaya wangu ambao nao wameanza kuchafuka kwa njia ile ile waliyonichafua na sasa wamejua kuwa magazeti ya udaku hayana urafiki yanauma na kupuliza.
Nawaomba wajitume na wasibweteke wasiendekeze majungu ya ngono, udini na ukabila wakae wakijua elimu ndio msingi wa kila kitu, ukielimika kamwe huwezi kuwa mtumwa wa fikra za woga. Haya ni maoni na ya mdau fulani nafikiri kwa kuyaweka humu atakuwa amefarijika kuwa blog hii imefanya kazi yake. Nami nimefurahi kuwaleteeni kero ya bw fulani toka Radio X ambayo ndiyo ya kwanza binafsi hapa nchini kama sikosei!
tuma kero yako yeyote humu mkala26@yahoo.com/ sambwe1295@gmail,com  nami nitaitupia humu bloguni.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

13 comments :

Anonymous said...

hata akificha jina tumeshamjua na hiyo ni radio one, yeye ndio mnafiki namba moja

Anonymous said...

jamani ama kweli yaliyomo yamo yaani watu hawana hata miwani ya maisha majungu yamekuwa ndo maakuli yao nadhani meseji imefika hapo atakayeguna uje limempata

Anonymous said...

kwe majungu makazini ni kero sana umenena ndugu yangu

Anonymous said...

nadhan kuna watu wanaingizwa makazini bila sifa stahiki na hao ndio vinara wa majungu na si makazini tu bali hata kwenye nyumba za ibada inakera sana

Anonymous said...

Jamani huyo binti ana matatizo asikimbilie kushutumu wenzake, kwanza hajui ethics za kazi zake ndio maana alithubutu kusoma msg ya kichochezi kutoka kwa msikilizaji na kutaka kusababisha kuvunja ndoa ya diwani mmoja wa CCM wa hapa Dar.

Anonymous said...

hayo ndo matatizo ya wanawake kutembea na mabosi zao baadae wanajiona untouchable hata wakifanya utumbo wanataka watu wakae kimya Times FM ulishindikana kwa sababu hiyo hiyo tunakujua sana
na wewe ndio bingwa wa kutukanisha watu magazetini

Anonymous said...

Hivi nyie mabinti wa Redio One kujiandika kwenye magazeti ya udaku ndio kutafuta umaarufu au kitu gani?

Anonymous said...

Hivi huyu anasema ni radio one ana ushahidi gani mbona radio ziko nyingi sana nchi hii au yeye ndio mlengwa? kama imekugusa jirekebishe

Anonymous said...

Radio Oneeee stereoooo!

Anonymous said...

HII NI KERO KUBWA POLE SANA MUNGU ATAKULINDA, PONGEZI SANA KWA HII BLOG HAPA NDIO UKOMBOZI WA SIE WANYONGE KEEP IT UP

Anonymous said...

POLE SANA SIKU ZOTE MCHAPA KAZI HUCHUKIWA

Anonymous said...

Unakimbia kivuli chako mama ni wewe uliyewananga wenzako kuwa hawajui KIINGEREZA ukasahau kuwa redio yenu inatangaza kwa lugha ya kiswahili hakuna aliyemkamilifu jali kilichokupeleka hapo usihangaike na maisha ya wenzako. ACHA HIZO.

Anonymous said...

Umeonaaaeee