News
Loading...

Vipi kuhusu Mwalimu?


Tabora station.
Mpendwa mdau leo nimetokea kukutana na rafiki yangu ambaye ni ofisa wa jeshi la polisi tukatokea kujadili masuala ya Jumuiya ya kimataifa na yanayotokea Libya. Mimi kwa kweli sioni kama kuna tatizo wa Libya wakitaka mabadiliko lakini si kwa hali hii inayoendelea, kwani sote tunajua zipo nija mwafaka za kufikia makubaliano. Rafiki yangu ana mtazamo tofauti anaunga mkono kumtoa Ghadaffi kama Amerika inavyofnya na wenziwe, wanatumia nguvu kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na ikiwezekana kumtoa kabisa kama si kumuua yule aliyepo madarakani kama Iraki. Rafiki yangu anasema "Ghadaffi lazima aondoke katawala muda mrefu sana pale Libya, hata kama yeye ndiye kiongozi wa nchi lakini anapaswa asilikilize matakwa ya wale wanaodai mabadiliko" Nami nakubali kuwa asemayo ni sawa lakini vipi hapa Tanzania? nani aliwasilikiliza wale waliokataa mfumo wa chama kimoja uliomuweka madarakani Mwalimu J.K. Nyerere madarakani kwa miaka yote 25 aliyotawala nchi hii? Sana sana waliambulia vifungo vya nje wasitoke maeneo ya majumbani kwao, hata walipotaka kwenda sokoni ilibidi waombe ruhusa kwa wahusika.Na hata sasa wale wachache au wengi waliodai katiba mpya hapa Tanzania wamekutana na vizingiti vingi kabla ya Mh Rais Kikwete kusema ataunda tume kujadili hilo. Tatizo letu wana wa adam tuna double standards kupita kiasi. Sasa mbona Tanganyika haikuingiliwa na mataifa ya nje kutaka iruhusu mfumo wa vyama vingi uendelee mara baada ya Uhuru, ni kwa sababu watu hawakupewa nafasi ya kueleza kwa uhuru yale walioyaamini, hivyo hawakusikika!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :