News
Loading...

Asiyekujua hakuthamini!


Hivi juzi nilipita Dodoma nikiwa njiani kwenda Tabora, nilibahatika kwenda iona Club 84, club maarufu na ya kisasa mjini Dodoma. Nikiwa ndani ya kilabu hicho kwa muda wa saa mbili hivi nikajisika kwenda msalani (short call), bahati niliposimama ni karibu na kaunta na nilikuwa nauona mlango wa choo cha kike nikategemea na cha kiume kitakuwa hapo pia. Nikipiga hatua mbili hivi huku nikichungulia nione ulipo mlango wa kile cha kiume ghafla nikasukumwa kurudishwa ninapotoka na baunsa ndipo kuumuliza kulikoni? akajibu "Toka, toka kwani hujui choo kikwapi? anasema huku akiendelea kunisukuma kwa fujo kabisa. Nikajaribu kumueleza kuwa mimi ni mgeni na sikufahamu hapakuwa na choo cha kiume mahala hapo. Hakutaka kunielewa kana kwamba aliambiwa namchukulia mkewe, wakati hata hatujuani. Kwa haraka yakanijia mawazo nikakumbuka kilichomtokea kaka yangu Swetu Fundikira nikawa mpole na nikajiondoa pahala hapo bila kuwa majeruhi. Nafikiri katika hali kama hizi jamani tujifunze kufikiri kitakachoweza kutokea mbeleni ili tuepuke ajali zinazoweza kutokea. Swetu Fundikira anadaiwa kuuawa na wanajeshi watatu baada ya kutokea kutoelewana barabarani kati ya dereva wa gari alilopanda Swetu na wanajeshi hao, kilichomponza Swetu ni kuamulia ugomvi huo.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :