News
Loading...

Kesi ya Swetu Fundikira Kuhamishwa leo!


Hayati Swetu Fundikira.
Kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira inayowakabili maaskari jeshi watatu sajin Rhoda Robert, Ally Ngumbe na Mohamed Ngumbe inatarajiwa kuhamishiwa mahakama kuu kwa kuanza rasmi kusikilizwa katika mahakama hiyo yenye uwezo wa kusikiliza na kuhukumu kesi za mauaji.Mnamo tarehe 21/01/2010 saa saba za usiku katika kona ya barabara ya Mwinjuma na Kawawa askari hao walimuweka chini ya ulinzi Bw Fundikira baada ya kutokea kutoelewana kati ya dereva wa gari ambalo Swetu alikuwa amepewa lifti na askari hao. Baada ya Dereva huyo kuzidiwa nguvu ndipo Swetu aliposhuka garini ili kuamulia ugomvi huo ambapo askari hao walilichukulia hilo kama kudharauliwa na Bw Swetu ndipo walipoanza kumshambulia wote watatu mpaka walipozingirwa na watu waliokuwepo maeneo hayo na kutaka maelezo toka kwa askari hao kwamba kwa sababu gani wanampiga ndipo wakatoa vitambulisho na kudai kuwa Swetu ni jambazi na alitaka kuwapora gari na kuwa wanampeleka Oysterbay Police ambako hawakumpeleka na matokeo yake wakakutwa naye maeneo ya Upanga jamatini akiwa hana nguo,viatu,simu,fahamu wala pochi yake ambayo ilikadiriwa kuwa na sh laki tatu na nusu. Na yote hayo yamewezekana baada ya taxi dereva mwenye moyo wa ki binadam kuwakuta watatu hao wakimshambulia bila huruma na ndipo alipoenda kituo cha polisi cha selander Bridge na kuwataarifu askari waliokuwepo hapo ndipo nao wakamuomba lifti awapeleke eneo la tukio.Kwa mipango ya Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliruhusu Swetu afe kifo kibaya hivyo, lakini pia Mwenyezi Mungu hakuruhusu wauaji wake watoroke bila kukamatwa na ndipo askari polisi toka Selander Bridge waliwakuta nae pahala hapo. Jana tarehe 24/01/2010 ilikuwa ni mwaka mmoja kamili tangu Mheshimiwa Swetu Fundikira kama akivyotambuliwa na wengi auawe kikatili. Mungu ilaze roho yake pahala pema peponi.! Amen.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :