News
Loading...

Kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira yapigwa tarehe!


Marehemu Swetu Ramadhani Fundikira.
Kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira inayowakabili askari jeshi watatu sajini Rhoda Robert, Ally Ngumbe na Mohamed Ngumbe haikuwezekana kuhamishiwa mahakama kuu leo hii baada ya kutokamilika kwa taratibu za kuihamisha. Akiieleza mahakama ya Kisutu hii leo mwendesha mashtaka Bi Monica Mbogo alisema upelelezi umekamilika lakini faili halijarudi toka kwa DPP ambako linatarajiwa kurudi Mahakamani Kisutu siku yeyote kuanzia leo ili kuhamishiwa mahakama kuu,hivyo kumuomba Mh hakimu Geni Dudu kuiahirisha kesi hiyo mpaka siku ya jumatatu ya tarehe 7/02/2011. Pichani ni ndugu na jamaa wa marehemu Swetu Fundikira. 
Wakatii huo huo:
Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja aliyekuwa mmoja wa wasikilizaji wa kesi hiyo alisikika akisema kama kuwabeza ndugu wa kike wa marehemu Swetu kwa kusema "Ndugu yenu jambazi ashakufa kinachowahangaisha nini? Kauli ambayo ilitaka kuzua kijizogo kabla ya busara kuchukua mkondo wake. Ambapo madada hao wa Swetu walisema wao wanachosubiri ni kuanza  kusikilizwa kwa kesi tu na si vinginevyo. Mwanamke aliyetoa kauli hiyo inaelekea ni ndugu wa watuhumiwa wa mauaji hayo kwani katika moja ya maelezo yao (watuhumiwa) Oysterbay police ni kuwa Swetu peke yake alikuwa jambazi aliyejaribu kuwapora gari wao askari jeshi watatu. Pia mama mmoja aliyesadikika kuwa  mama wa watuhumiwa alisikika akimwambia mpiga picha wa ITV " Siku zote mlikuwa wapi hadi mkaona mje leo? Mpiga picha huyo wa ITV hakuonekana kumsikia mama yule kwani aliendelea na kazi yake kama kawaida. Kwa mujibu wa askari polisi wa Selander bridge na wale wa Oysterbay Marehemu Swetu hakukutwa na silaha ya aina yeyote. Hata hivyo pamekuwa na malalamiko juu ya usomwaji wa kesi mbali mbali mahakamani hapo, kwani waendesha mashitaka, karani na mahakimu hawaoneshi kuthamini uwepo wa wa waskilizaji kwa kuongea kwa sauti ya chini mno jambo ambalo limewafanya wafuatiliaji kutoskia kinachozungumzwa juu ya  kesi na kupelekea kuulliza kimesemwa nini au kesi imeahirishwa mpaka lini. Nafikiri inabidi wahusika walitilie maanani hili ili wasikilizaji waweze kwenda sambamba na mienendo ya kesi mahakamani hapo.

Madada wa Swetu Fundikira wakisubiri kutajwa kesi.

Ismail Fundikira, Nzwala Fundikira, Msabila Fundikira na Ipyana Mwandembwa.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :