News
Loading...

Tanzania Dance Music Competition!


Hii ni nembo ya Tanzania Dance Music competition
Ndugu wadau leo itabidi mniwie radhi kwani ninachofahamu kuhusu hizi picha ni kuwa hawa vijana pichani wanagombea nafasi za kuchukuliwa kuimba katika Bendi kubwa za Muziki wa Dansi hapa nchini. Kwa kifupi shindano hili linawashindanisha wanamuziki chipukizi wa muziki wa dansi tu. Nilifika Msasani club ukumbi wa ndani ambapo ndipo shindano hilo linafanyikia kwa bahati tu sikuwa nimealikwa lakini ulipofikia muda wangu wa kuondoka nikaona haitokuwa vibaya kuwarusha vijana katika blogu hili nikachukua picha zao na hatimaye ikabidi nipate walau machache ya kunogeshea habari hii kutoka kwa muandaaji. Kwa bahati nzuri shindano lilikuwa limesimamishwa kwa mapumziko mafupi hivyo ulikuwa wasaa mzuri kuongea na muandaaji wa shindano hilo chipukizi. Bahati mbaya kwangu Bwana huyo hakutaka hata kujua mimi ni nani na nataka kumhoji kwa sababu gani.
akajibu tu katika hali ya ghadhabu " Niacheni nimalize ndio nikae chini kujibu maswali" Nikabaki nimeduwaa mdomo wazi nisiamini kinachotokea, anyways nilikuwa naondoka so i left. Ndio sababu habari hii haijakamilika, lakini nawaahidi leo mchana nitakuwa nimepata maelezo zaidi juu ya mpambano huu. Kwa jinsi nilivyoona ni shindano zuri ambalo likipata mdhamini litakuwa tishio hapa nchini. Kingine nilichopenda ni watu waliohudhuria kuanzia King Ki Ki, Asha Baraka, Waziri wa Njenje, Ally Choki akiwa kama jaji mmojawapo pamoja na viongozi kadhaa wa CHAMUDATA inaonesha waandaaji wamejipanga vilivyo ila nina angalizo itawabidi waboreshe sekta ya Uhusiano na wajue nini cha kumjibu nani wakati gani, wakirekebisha hilo watafika mbali. Siku kama ya leo ningekuwa nawakilisha kampuni fulani iliyonituma kuangalia uwezekano wa kudhamini mashindano hayo ningerudi kwa wakubwa zangu na majibu gani, kama si "Ah wale bado sana kwanza hawajui kuimba halafu hawana nidhamu, kama mtayarishaji wa shindano kama lile hana nidhamu basi ujue na washirki watakuwa hawana nidhamu pia. Na ningemalizia nafikiri tusiwape udhamini tusije kulaumiana bure hapa" Kwa kauli kama hiyo ya mpambe nuksi si basi tena hakuna udhamini.
,
Hawa ni washiriki wote wa shindano hilo.

Hawa ni The Masauti Band.

Hii ni Pili Pili Band.

Mr Waziri wa Njenje alihudhuria.

Mkurugenzi wa ASET Bi Asha Baraka akibadilishana mawazo na King Ki ki


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :