News
Loading...

Tigo na Vodacom mnatusumbua wakazi wa KinondoniKampuni za simu za mkononi za Tigo na Vodacom zimekuwa zikitupa usumbufu wateja wao tunaoishi maeneo ya Kinondoni, kwa kutokuwa na ofisi katika maeneo haya, hivyo hata ukinunua vocha ya sh 500 na ikagma kuingia katika kilongalonga chako itakubidi upande daladala mpaka posta au Mlimani city ambako ndipo ofisi zao zilipo kwa sasa. Tigo wao waliwahi kuwa na ofisi Mayfair Plaza lakini kwa sababu wanazozijua wao wakaiondosha ofisi ile jambo ambalo linatupa karaha sisi tunaowaweka mjini, sijui ule msemo wa mteja mfalme hawaujui au wanachojaribu wao ni kutukamua tu huku wao wakiingiza faida tele kwa tele. Nikiwa kama mmoja wa wateja wao nawaomba waweke ofisi katika maeno haya ili watupunguzie safari za mjini na Mlimani city.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :