Jeneza la marehemu Kanumba likiwasili ktk viwanja vya Leaders
Umati mkubwa umejitokeza leo hii katika viwanja vya Leaders ukiongozwa na Makamu wa Rais Mh Dk Gharib Bilal ili kutoa heshima za mwisho wa kwa aliyekuwa msanii nguli wa sanaa ya maigizo nchini Tanzania marehemu Steven Kanumba. Hapo leaders watu wamejaa kiasi kwamba wengine hawaruhusiwi kuingia na hii inatokana na kuchelewa shuhuli ya utoaji heshima za mwisho. Sidhani kama kuna raia wa Tanzania au hata kiongozi wa serikali amewahi kupata umati mkubwa kama huu labda Mwalimu J.K. Nyerere. Umati huu na uwe njia nyepesi kwake kuelekea mapumzikoni.
0 comments :
Post a Comment