News
Loading...

Mshahara wa mbunge ni sawa mishahara ya miaka mitatu ya mwalimu


Mh John Shibuda Mbunge pekee wa CHADEMA
anayetetea maslahi nono ya wabunge.
Imeelelezwa kuwa baada ya wabunge kupandishiwa posho za vikao, sasa mishahara yao ya mwezi inaweza kumlipa mwalimu kwa miaka mitatu. Hivi karibu Mh Spika Anne Makinda alitangaza kupandishwa kwa posho za wabunge kwa siku kutoka sh 70,000/= mpaka sh 200,000/=. Hatua hiyo imeibua jazba miongoni mwa walala hoi ambao kila siku inakuwa ni afadhali ya jana, jinsi hali ya maisha inavyokuwa mbaya, huku mfumuko wa bei nao ukiendelea kushamiri. Uchunguzi uliofanywa na gazeti moja la kila siku umebaini kuwa  mbunge hulipwa mshahara wa sh 7,300,000/= ( Milioni saba na laki tatu). Mwalimu wa shule ya msingi katika daraja la TGTS B ni sh 200,000/= kwa mwezi. Na kwa mwalimu wa sekondari mwenye shahada na daraja TGTS C mshahara wake ni sh 300,000/= tu. Mishahara hii ni kwa wale wanaoanza kazi. N a mchanganuo huo unaonesha kuwa mishahara hiyo ni kabla ya kukatwa kodi yeyote ile.
Hii ni dhahiri kuwa wabunge hawana machungu yeyote juu ya hali ngumu ya kimaisha ya wa Tanzania walio wengi.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :