News
Loading...

Kipindupindu chavamia Tabora!


Maafisa wa idara ya AFYA.
Lililokuwa shimo la taka limejaa maji.

Mahanjumati yakitayarishwa.
BREAKING NEWS! Napiga kikombe, cha chai lakini!


Kwa dada hakuna uosefu wa mahitji muhimu!
Kwa mujibu wa Maafisa wa Idara ya Afya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tabora ameripotiwa mgonjwa mmoja wa kipindupidu kalazwa katika Hospitali ya Mkoa Kitete, hivyo walifika maeneo ya kwa dada kukagua na kutahadharisha kuhusu gonjwa hilo hatari. Na kwa hali ilivyo maeneo hayo lilikuwa ni jambo la busara kwao kufika maeneo hayo na kutoa tahadhari. Mbele ya nyumba moja inayotazamana na ya dada pana akina Mama Lishe ambao wana banda karibu na shimo la taka lililogeuka kuwa shimo la maji machafu kufuatia mvua iliyonyesha jana usiku, maafisa hao walimfuata mwenye nyumba hiyo na kumwambia afukie shimo hilo haraka iwezekanavyo huku wakiwa wameandamana na Mwenyekiti wa mtaa wa Urban Quarter Bw Masumbuko Bakari. Katika hatua nyingine nilidadisi bei za vyakula mahala hapo nikabaini, wachuuzi wote bado wanatoza bei ya kawaida ambayo ni sh 1500 kwa wali nyama, kikombe cha chai ni sh 100 mpaka sasa, lakini wakalalamikia ukosefu wa wateja na kusema watu wengi hapo kwa dada ni wakazi wa Tabora na hufika hapo na vyakula vyaohivyo kuwafanya wabaki na vyakula!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :