News
Loading...

Kuenguliwa kwa Sitta ulezi wa UVCCM Tabora kwazua utata.


Sakata la kumuengua mlezi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Samuel Sitta, limezua utata baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Iddy Ally, ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya UVCCM Tabora kumkana Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga, aliyetangaza uamuzi huo. Bw Iddy Ally amesema hana taarifa za kuenguliwa kwa Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Akizungumza jana katika ofisi za UVCCM mjini Tabora, Ally alisema yeye kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya UVCCM, hana taarifa za kuenguliwa kwa Sitta na taarifa hizo zimemshangaza.
Mh Samuel John Sitta.
Alisema taarifa hizo alizisikia kupitia vyombo vya habari, bila kujua kikao gani kilitoa tamko hilo. “Jumuia ya vijana inapotaka kufanya vikao, lazima nipewe taarifa na nihudhurie. Mimi kwa sababu ni mjumbe wa kamati tendaji. Jambo hilo silijui. Alisema taratibu za maamuzi mbalimbali ndani ya chama zinaenda kwa vikao ambnavyo huhudhuriwa na wajumbe wote wa kamati ya utendaji ili kuondoa utata unaoweza kujitokeza. 
Alisema anasubiri Katibu wa UVCCM Mkoa, Julius Peter, ambaye yuko safarini ili kupata maelekezo kuhusiana na taarifa hizo.
Jumatano wiki hii, Bw Robert Kamoga alitangaza kuenguliwa kwa Sitta kwa madai kuwa amekidhalilisha chama kwa kusema UV-CCM mkoa wa Tabora inateswa na siasa za makundI. Mh Sitta amekuwa akipingwa katika misimamo yake mingi ndani ya CCM kwa kile kinachoelezwa kujitafutia umaarufu kwa kukemea masuala anayoamini hayapo sawa au yasiyo na maslahi kwa mwananchi wa kawaida. Na misimamo hiyo imemfanya kuwa adui nambari moja ndani ya CCM ambapo imepelekea kuenguliwa ki mizengwe katika kugombea uspika.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :