News
Loading...

Tamasha la Seco college Tabora lafana!


Msanii Samir akifanya vitu vyake jukwaani.
Tamasha la Seco College lililofanyika jana katika uwanja gofu wa Ally Hassan Mwinyi lilifana kwa kiasi kikubwa, tamasha hilo lilioandaliwa na vijana wazalendo wa mkoa huo TEA lilipambwa na wasanii 20Percent, Juma NatureSamir, Sharobaro na Belle9 pamoja na kundi la wacheza kiduku wa kundi la Pakacha. 20Percent ambaye baadae usiku wa jumamosi alijishindia tunzo tano za Kili Music 2011 ndiye alikuwa nyota wa Tamasha hilo, alikonga nyoyo za maelfu ya washabiki  waliohudhuria uwanjani hapo, Nyota huyo wa Bongo Flava ametokea kuwa kipenzi cha wapenzi wa muziki wa rika zote kutokana na umahiri wake wa kuandika na kuimba mashairir yenye maana, na si ajabu kwangu mimi yeye kuzoa tunzo hizo tano. Hata hivyo kasoro ndogo ilijitokeza baada ya umeme kukatika mjini Tabora huku Juma Nature akiwa hajapanda jukwaani, lakini baada ya saa moja hivi umeme ulirudi na akapanda jukwaani kutumbuiza. Hili ni funzo kwa waandaaji wa Tamasha hilo ambao hawakuwa na genereta standby, kwa mgao uliopo nchini hivi sasa walipaswa wawe nalo kwa akiba. Big up!
Hawa ni kati ya maelfu ya wakazi wa Tabora waliofika Mwinyi stadia.
Wakazi wa Tabora  Mgalula Fundikira na Zaudito Balkis.

Samir akibadilishana mawazo na mashabiki wake baada ya kutumbuiza.


Belle9 akishambulia jukwaa.

Dah watu wote hawa, lazima jamaa wamepiga hela!

Zaudito na mshkaji ambaye jina lake halikupatikana.

Huyo Zaudito vipi? kila picha yumo! kulia ni Jackie

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Anonymous said...

cool