News
Loading...

Hongera Kili Music Awards, lakini!


Man Water.
Nikiwa mmoja wa wana akademi 100 tulioteua nominees nina furaha kuona sasa angalau matatizo na malalamiko yanapungua katika tunzo hizo. Lakini kuna jipya limejitokeza, ni vipi Man Water akose tunzo? ilihali msanii alimtengenezea albam nzima kashinda tano? Hapa pana tatizo na ni vema mwaka kesho lisijitokeze tena. Kama mwana akademi naelewa kivipi hili limetokea, lakini napenda kupendekeza mwaka kesho ikitokea msanii mmoja kashinda tunzo tatu au zaidi na nyimbo hizo tatu kama kafanyiwa na mtayarishaji mmoja basi automatically mtayarishaji husika apewe tunzo ya mtayarishaji bora. Na ikitokea wametokea wasanii zaidi ya wawili wamepata tunzo 3 basi watarishaji hao washindanishwe apatikane mmoja wa kupata tunzo hiyo ya mtayarishaji bora. Yote na yote kwa vyovyote Water anajisikia kama ni mshindi wa tunzo ya mtayarishaji bora wa muziki, na mimi ningekuwa ndiye niliyepwa tunzo hiyo ningempa Water, aibu jamani!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :