News
Loading...

Je tuna ulazima wa kuwa na wazee wa baraza mahakama kuu?Mahakama kuu wiki iliyopita.
 Tangu wazee wa baraza watoe maoni tofauti mno na mwenendo na ushahidi katika kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira, ambapo waliwakosa na hatia washtakiwa wote watatu, nimekuwa nikijaribu kuueleza umma juu ya kile ninachofikiri juu yao. Kwa kweli nafahamu nyote msomao makala hizi mnaelewa uhusiano wangu na marehemu Swetu Ramadhani Fundikira kwani mimi ni Mkala Ramadhani Fundikira.
Siku ambayo Mh Jaji Mruke alipowapa nafasi wazee wa baraza kutoa maoni yao juu ya kesi hiyo kabla ya kuwaruhusu kuongea aliwapa somo ni jinsi gani wataweza kupata maoni yao na alianza na kusemaili kesi ya mauaji iwepo na mshitakiwa athibitike ni lazima pawepo na mambo manne(4) muhimu

1.Ithibitike marehemu amefariki
2.Awe amekufa kifo kisicho cha kawaida (not natural death) 
3.Ithibitike washitakiwa ndio waliosababisha kifo
4. Je, kulikua na NIA OVU?

Katika haya manne nitayatolea majibu moja baada ya jingine kama ifuatavyo:

1.Ithibitike marehemu amekufa:
Polisi na daktari walithibitisha kuwa Swetu Fundikira alikufa hospitalini MOI tarehe 23/01/2010.
2.Awe amekufa kifo kisicho cha kawaida:Swetu alikufa kifo kisicho cha kawaida tena ni cha kinyama huku akiachwa uchi wa mnyama.
3.Ithibitike watuhumiwa ndio waliosababibisha kifo chake:
Washtakiwa wote watatu pamoja na kuwa hawakuonekana wakimuua Swetu, lakini wenyewe wanakiri kuondoka naye Kinondoni akiwa na hali nzuri kiafya na wanakiri kukutwa naye huko Upanga na Polisi akiwa uchi na asiyejitambua na mwenye majeraha mengi ya kichwa. Je nani aulizwe juu ya kifo cha Swetu?
4.Je kulikuwa na nia ovu?:
Kuhusu kuwepo kwa nia ovu ni dhahiri ilikuwepo, ni vp marehemu alikuwa na majeraha kichwani tu? Hii inaonesha kipigo alichokuwa akipewa kilidhamiriwa kipelekee maumivu yenye madhara kwa marehemu. Vile vile mshtakiwa namba 1na wenzie wanapoondoka na marehemu Kinondoni na kusema wanampeleka Oyserbay Police kama alivyomwambia Ben Kinyaia na baadae kwenda nae kwingine na kuviruka vituo kadhaa vya polisi hii pia ni ishara ya nia ovu.

Labda hapa sasa nirudi kwa wasomaji wangu, je? wazee wale wa baraza ni kipi ambacho hawakukielewa kiasi cha kuwakosa na hatia washtakiwa katika mambo yote manne yaliyoelezwa na Mh Jaji Mruke ni lazima yathibitike? Na kama hawakuelewa basi hata busara hawana? Kama ni hivyo, Je kuna sababu ya kuwa na wazee wa baraza katika mahakama zetu hasa zile kuu?

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :