News
Loading...

Kama akifungwa chini ya miezi sita atarudi mjengoni? Masihara hayo!


Mbunge wa Bahi Mh Omari Badwel akisindikizwa na askari
Wiki kadhaaa zilizopita tulishuhudia mbunge wa Bahi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mh Omari Badwel akifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa, na baadae tukaja kusoma na kusikia katika vyombo vya habari kuwa Mh Badwel hata akipatikana na hatia na akafungwa jela kwa kifungo kisichozidi miezi 6 akitoka ataendelea na wadhifa wake wa kuwawakilisha wananchi wa Bahi. Na hiyo ndiyo taratibu sahihi iliyowekwa na wahusika. Sasa mimi najiuliza, Mh sana Bw Badwel au mbunge yeyote atakayefungwa jela kwa kupatikana na hatia ya kula rushwa hata ikiwa kwa siku moja tu gerezani ni kweli atafaa kurudi kuongoza wananchi? Hapana, mimi naona iwapo mbunge atapatikana na hatia ya kula rushwa na mahakama basi kiti chake kiwe wazi naye asiruhusiwe kugombea kiti hicho au chochote kingine nchini. Hapo tutakuwa tumefanya jambo zuri na lenye kuwatendea haki wapiga kura na mbunge husika atakuwa si ameadhibika kwa kifungo tu bali kukosa ubunge ambao tunavyofahamu huwaneeemesha sana waheshimiwa.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :