News
Loading...

Kutekwa, kuteswa, kupigwa na kujereuhiwa Dr Ulilmboka kuna harufu ya faulo!


Dk Ulimboka Steven baada ya kukotwa
Nchi ya Tanzania imeshuhudia tukio la kinyama na la Ki mafia kuliko yote yaliyopata tokea hapa nchini. Kutokana na kuendelea kwa mgomo wa madaktari nchini nani hatokuwa na wasi wasi kuwa kutekwa, kuteswa na hatimaye kupigwa kinyama kwa Dr Ulimboka Steven ambaye ni mwenyekiti wa umoja wadaktari nchini, umoja ambao ndio unaongoiza mgomo wa madaktari. Tumepata kusikia minong'ono kuwa viongozi wengi wa chama na serikali waliokwenda kinyume na matakwa ya wakubwa wao ama walikufa katika mazingira ya kutatanisha au walienda gerezani kunyea debe. Mifano hai ipo na mwingine hivi sasa ni kiongozi mkubwa tu hapa katika Jamuhuri ya Muungano. Suala la kunyofolewa kucha Dr Ulimboka inaonesha wazi waliomtesa ni watu wenye mafunzo ya kutesa watu na wanaojua wanachokifanya, Je cha kujiuliza wewe msomaji wangu watu aina hiyo wanapatikana katika viwanda vya watu binafsi au katika idara nyeti za usalama ambazo huwa chini ya serikali? Hata sijui tunaendea wapi na vitendo hivi vya ki Mafia. Tukio hili linarudisha nyuma mpaka mwaka Jan/2010 ambako kaka yangu Swetu Fundikira alitekwa nyara na askari jeshi watatu kutoka maeneo ya Kinondoni na saa moja baadae wakakutwa naye maeneo ya Upanga jamatini akiwa uchi wa mnyama na hana fahamu kwa kipigo na baadae alifariki hapo Muhimbili Hospital kwa majeraha ya kichwa.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :