News
Loading...

Conservatives si chama cha wageni England, Tusikipe kura zetu!


David Cameron waziri mkuu wa UK
Chama Tawala kinachoiongoza United Kingdom cha Conservatives kinachoongozwa na Bw David Cameron kwa kupitita serikali mseto na chama cha Liberal Democrats kinachoongozwa na Nick Clegg baada ya vyama vyote viwili vikubwa vya nchi za umoja wa falme hizo za ki British yaani Labour Party na Consevervative kushindwa kupata ushindi mnono wa kuviwezesha vyama hivyo kuunda serikali. Hali hiyo ilipelekea  Conservatives kuungana na Liberal Democrats kulazimika kuungana ili kufikisha idadi ya viti vilivyoviwezesha vyama hivyo kuunda serikali na hivyo Labour Party kukaa pembeni baada ya kuingoza nchi hiyo kwa miaka 10 mfululizo kupitia Tonny Blair miaka 8 au 9 hivi na kisha Gordon Brown miaka iliyobaki. Cha kushangaza hawa Liberal Democrats au (Lib dem) kwa kifupi hawakutaka kabisa kuungana na Labour party labda kwa kuhofia kumezwa au kwa sababu nyingine wazijuazo wao, na wao Lib dem na Labour sera zao hufanana sana kiasi kwamba wadau wa siasa za nchi hiyo walipata kuwashauri Lib dem kwa kejeli kwa nini isijiunge na Labour kwani sera zao ni moja. Nirudi katika kichwa cha habari, hawa Conservatives katika kampeni zao walieleza wazi wazi kuwa wao watawabana wageni na wahamiaji, na kuwa wangeongeza ada za elimu hasa ile ya juu na pia wangepunguza masaa ya kufanya kazi wanafunzi wageni kutoka 25 mpaka 10 kwa wiki. Kwa mfano kwa sasa waombaji wa mikopo kwa elimu ya juu wameshuka kwa asilimia 40 kwani Conservative imepandisha ada kutoka pauni 4500 mpaka pauni 9000, ongezeko la karibu asilimia 100. Kana kwamba hiyo haitoshi pia wamepunguza masaa ambayo mwanafunzi atafanya kazi na kujipatia pesa za kujikimu kutoka saa 25 kwa wiki ambazo ni sawa na pauni 150 hadi saa 10 kwa wiki ambazo ni sawa na pauni 58 baada ya kodi ya mapato kukatwa. 

Sidhani kama unahitaji kuwa mwaanasayansi wa nyuklia kujua watu hawa Conservatives hawataki wageni nchini mwao, cha msingi ni wageni kuamka na kutowapigia kura ili wasirudi madarakani katika uchaguzi ujao. Ipe kura yako Labour Party

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :