Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson jana alilazimika kumuomba msamaha mlinzi nguli wa timu hiyo na Manchester United RioFerdinand baada ya kusema kuwa Rio Ferdinand hatoichezea tena timu hiyo ya taifa, aliyasema hayo akijibu swali la mshabiki mmoja wa soka aliyetaka kujua kama Rio angejumuishwa katika kikosi kipya cha England. Hodgson ambaye alimuacha Rio nje ya kikosi cha England kilichoshiriki Euro 2012 nchini Poland na Ukrayne kwa kuwa mdogo wa Rio, Anthon amekuwa na na kesi dhidi ya John Terry ya kumdhalilisha kibaguzi wa rangi katika mchezo kati ya Chelsea na QPR mwaka jana. Hivyo Hodgson akaona asingeweza kuwachagua Rio na Ferdinand kuichezea England kwa pamoja. Lakini akatoa sababu kuwa amemuacha Rio kwa sababu za kimchezo (Football reasons). Kana kwamba yote hayatoshi kumuumiza Rio, Hodgson amekuwa akimpa sapoti kubwa John Terry wakati wa kesi yake dhidi ya Anthon Ferdinand jambo ambalo kama kocha wa timu ya taifa hakupaswa kuchagua upande wa kupendelea. Faragha Rio amekuwa akisononeka juu ya hilo lakini alipofikia kusema kuwa Rio hatoichezea tena England tena kabla hajamwambia mwenyewe Rio imepelekea yeye kuona kuwa Hodgson ana chuki binafsi dhidi yake na ndipo Roy Hodgson akalazimika kumuomba msamaha Rio na kukanusha kuwa hakumaanisha kuwa hatomchagua tena Rio kuichezea England. Sakata hili ni mtiririko tu wa vituko ambavyo Rio amefanyiwa ama na England, meneja wa zamani Fabio Capello au FA yenyewe. Makala hiyo itawajia karibuni hapa hapa.
0 comments :
Post a Comment