News
Loading...

Vituko vy Fabio Capello dhidi ya Rio


Fabio Capello
Baada ya John Terry kuvuliwa unahodha wa timu ya taifa ya England kabla ya timu hiyo kwenda South Africa kwa kile kilichoelezwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie Wayne Bridge (mpenzi wa zamani). Wayne Bridge alikuwa akichezea Chelsea kama ilivyo John Terry na pia wawili hao walikuwa marafiki. Unahodha huo alipewa Rio Ferdinand na kocha Fabio Capello. Kwa bahati mbaya kabla mashindano hayajaanza huko South Africa, Rio akaumia mazoezini, hiyo ikapelekea unahodha huo apewe Steve Gerrard kwa muda. Baada ya mashindano kwisha na England kuwa imeboronga vya kutosha. Baada ya hapo Capello akawa anawashwa kumrudishia unahodha huo John Terry na hatimae akamrudishia na hilo liliwezekana kirahisi baada ya Rio kuwa majeruhi mara kwa mara. Hata Capello alipoamua kumrudishia John Terry unahodha huo pia hakuwa na ustaarabu wa kumfahamisha nahodha aliyepo kwa wakati huo yaani Rio Ferdinand kuwa kwa sababu kadha wa kadha ameamua kumrudishia unahodha huo John Terry. Masikini ya Mungu Rio akayasikia hayo kupitia vyombo vya habari kama mimi na wewe. Pamoja na kuwa ameichezea timu hiyo mara 81 lakini hakuoneshwa heshima wala kuthaminiwa si na Capello wala FA. Baya zaidi ni kuwa pamoja na kuwa Capello alikuwepo Old Trafford lakini hakufanya jitihada yeyote kumtafuta Rio na kumpa sababu zake za kumpoka unahodha. Rio akabaki akisononeka. Na kana kwamba hayo yote hayakutosha kwa Rio Fabio Capello alitakiwa na FA amvue unahodha John Terry kwani FA haikutaka kwenda katika Euro 2012 na nahodha anayetuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi. Fabio akagoma kuchukua hatua hiyo na akaamua kujiuzuru ukocha wa timu hiyo. Ndipo akapewa Hodgson kazi hiyo. Ambaye naye bila ajizi akamtema Rio na kubaki na Terry ma baadae Terry alipokuwa akikabiliwa na kesi ya ubaguzi dhidi ya Anthon Ferdinand kwa FA baada ya mahakama kumkosa na hatia kitatanishi, Hodgson bila haya hata chembe akawa anamtetea Terry kwa kumpamba na kudai kuwa asingepatikana na hatia kama ambavyo mahakama ilivyomkosa na hatia. Hapa Rio akiwa na mawazo kuwa Hodgson aliamua kumtema yeye na kumtetea sana Terry kwa kuwa ni mweupe na anashtakiwa kwa kwa kesi ya ubaguzi atakuwa amekosea?

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :