News
Loading...

Kero ya mizani Kibaha Serikali itafute njia mbadala


Msururu wa magari yakisubiri kukwamuliwa yalekee Dar
Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mwasiliano na uchukuzi au na ile ya ujenzi kwa uoja wao wanapaswa kama hawajafikiria basi wafikirie njia mbadala itakayopunguza kero ya misururu isiyo na msingi pale Kibaha mizani. Kwa mfano ikifika saa 11 jioni hujakatikaza pale basi utajuta kupajua Kibaha mizani, tatizo ni kuwa malori mengi huanza safari jioni na yote hayo hutokea Dar kwenda mikoani na nje ya nchi  kama Rwanda, Burundi, kenya, Uganda nk, foleni ya malori huwa na urefu hata wa kilometa 2 hivi, sasa kuna wale wenye gari ndogo ambao hawaoni kwa nini wapange foleni wakati hawana haja ya kupima gari zao? Ndipo huingia katika pande ya kulia kwao ambayo hutumika na magari  yatokeayo mikoani kuelekea Dar, ndipo hapo msongamano unapoanzia. Sidhani kama panahitajika maprofesa waje kutafiti nini tatizo ni kiasi cha serikali kuitanua barabara hiyo japo iwe na njia sita, tatu zinakwenda na tatu zinarudi. Pia ningependekeza katika hizo njia tatu kuwe na moja iliyotengwa rasmi kwenda mizani na ianzie km3 kabla ya kufika mizani. Hapo nafikiri adha hiyo ya kukwama katika foleni Kibaha mizani itakwisha, fikiria umetokea mkoani kwa shuhuli yeyote ile ukitarajia kufika Dar saa 10, kwa hali ilivyo sasa utafika saa 12 jioni. Ni hayo tu kwa leo
Msururu huu ulikuwa na urefu wa kilometa 2



FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :