News
Loading...

Liverpool inamuunga mkono Luis Suarez


Luis Suares akifanya mazoezi mepesi na wachezaji wenzie
Timu ya Liverpool  na kocha wao Kenny Dalglish jana kabla ya mchezo wao na Wigan walivaa fulana zenye picha ya Luis Suarez na mgongoni zikiwa na nambari saba ambayo ndio namba aitumiayo Luis Suarez hapo Liverpool. Hatua ya hiyo ya Liverpool ni kuonesha mshikamano na mchezaji wao huyo ambaye amepatikana na hatia ya kutumia lugha ya kibaguzi dhidi ya mchezaji wa Manchester United Patrice Evra siku timu zao zilipocheza katika uwanja wa Anfield. Suarez amelalamikiwa na Evra kuwa alimwita Evra Negro zaidi ya mara kumi. Chama cha soka cha England kilifanya uchunguzi wa tuhuma hizo kwa kipindi cha takriban miezi mitatu na hatimae kumpata na hatia Luis Suares na kisha kumuadhibu kwa kumfungia kucheza mechi 8 na faini ya pauni za kiingereza 40,000, na amepewa siku 14 kukata rufaa. Adhabu hiyo imepingwa vikali na klabu ya Liverpool na wanjipanga kukata rufaa. Baada ya timu ya Liverpool kuvaa fulana hizo pamekuwa na malalmiko kadhaa toka kwa wacheza mpira wa zamani hasa weusi ambapo wameeleza kusikitishwa na kitendo hicho ambacho wamekiita ni kama kuunga mkono maneno ya kibaguzi yaliyotumiwa na Luis Suarez dhidi ya Patrice Evra. Pia waliongeza kama waliona kuna sababu ya kuvaa fulana basi wangevaa fulana zinzopinga vitendo vya kibaguzi na si fulana hizo ambazo zimeiweka klabu hiyo katika mtazamo mbaya hasa kwa wana harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :